Na Mwandishi Wetu
BONDIA Ibrahimu Tamba anapanda tena uringoni Novemba 22 katika ukumbi wa Frends Corner Manzese Dar es salaam kugombania mkanda wa ubingwa na bondia Baraka Mwakansope kutoka Mbeya kg 73 mpambano uho wa raundi kumi
unatalajiwa kuwa wa kisasi baada ya mara ya kwanza Tamba kumsambalatisha bondia Maisha Samsoni wa uko uko Mbeya hivyo mwakansope amekuja kwa ajili ya kulipiza kisasi cha kupigwa kwa mwenzake mpambano uliofanyika mwanzoni mwa mwaka huu
mratibu wa mpambano uho Jaffar Ndame ameongeza kwa kusema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mawili ya ubingwa ambapo bondia Julius Kisalawe atapambana na Ramadhani Kumbele kg 51 ubingwa wa Taifa mpambano wa raundi kumi
mpambano mwingine utawakutanisha bondia Pius Kazaula wa Morogoro atakaepambana na Abdallah Luwanje wakati bondia chipkizi kutoka Super D Boxing Promotion Vicent Mbilinyi atakabiliana na Said Tampoo kutoka bagamoyo
aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine ya mabondia chipkizi mbali mbali pia kutakuwa na burudani za kutosha hivyo kawaomba wapenzi na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuwai ukumbini kwa michezo itanza rasmi kuanzia saa 11 jioni na kumalizika mnamo saa tano kasoro usiku
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
No comments:
Post a Comment