Shirika la Taifa la Hifadhi yaJamii(NSSF)
limetoa Elimu kwa Wenyeviti na Makatibu wa Wakulima wa Korosho na Ufuta wa Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi kuhusu mpango wa
Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima, Mpango huo unamwezesha mkulima kupata mikopo
mbalimbali ikiwemo mkopo wa vifaa vya kilimo pamoja na pembejeo za kilimo.
Aidha mpango huo unamwezesha mkulima na familia
yake kufaidika na mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF yakiwemo mafao ya matibabu
ambapo mkulima atapata matibabu bure yeye na familia yake.
Wanyeviti na Makatibu hao waliweza kuuliza maswali na kupata
ufafanuzi wa kina kuhusu Mpango huu kwa Wakulima na jinsi ya kuwasaidia Wakulima
kuondodokana na gharama za matibabu kupitia mafao ya matibabu yatolewayona na NSSF.
Wakulima wa Korosho wa Kilwa Masoko wakiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa NSSF baada ya kumalizika kwa Semina.
Afisa Ushirika wa Vyama vya Wakulima (AMCOS) Bwana
Vincent Mhengilolo akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Ushirika
wakati wa Semina iliyoandaliwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii(NSSF)
Mkulima wa Korosho wa Kilwa Masoko akiuliza swali ili
kupata ufafanuzi kuhusu Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima Mjini Kilwa
Masoko.
Afisa Mafao wa Shirika la Taifa la Hfadhi ya Jamii NSSF Bi Lydia Ignas akitoa ufafanuzi kuhuhu mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Lindi Bi Nour Azin akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Wakulima kuhusu mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima katika semina iliyofanyika Kilwa Masoko Mkoani Lindi.
Ofisa Mafao wa NSSF, Kabonwa Kandoro akiwaandikisha uanachama Wenyeviti na Makatibu wa vyama vya wakulima AMCOS baada ya semina iliyofanyika Kilwa Masoko mkoani Lindi.
Ofisa Mafao wa NSSF, Kabonwa Kandoro akiwaandikisha uanachama Wenyeviti na Makatibu wa vyama vya wakulima AMCOS baada ya semina iliyofanyika Kilwa Masoko mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment