Shirika la Taifa la Hifadhi yaJamii(NSSF) limetoa Elimu kwa
Wenyeviti na Makatibu wa Wakulima wa Korosho na Ufuta wa Wilaya ya Kilwa Mkoa
wa Lindi kuhusu mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima, Mpango huo unamwezesha
mkulima kupata mikopo mbalimbali ikiwemo mkopo wa vifaa vya kilimo pamoja na
pembejeo za kilimo.
Aidha mpango huo unamwezesha mkulima na familia yake
kufaidika na mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF yakiwemo mafao ya matibabu
ambapo mkulima atapata matibabu bure yeye na familia yake.
Wanyeviti na Makatibu hao waliweza kuuliza maswali na kupata
ufafanuzi wa kina kuhusu Mpango huu kwa Wakulima na jinsi ya kuwasaidia
Wakulima kuondodokana na gharama za matibabu kupitia mafao ya matibabu
yatolewayona na NSSF.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Lindi, Nour Aziz akizungumza na
Wenyeviti na Makatibu wa Vyama vya Wakulima kuhusu mpango wa
Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima katika semina iliyofanyika Kilwa Masoko Mkoani
Lindi.
Ofisa Mafao wa Shirika la Taifa la Hfadhi ya Jamii
NSSF Bi Lydia Ignas akitoa ufafanuzi kuhusu mafao mbalimbali yatolewayo na NSSF.
Mkulima wa Korosho wa Kilwa Masoko akiuliza swali ili kupata
ufafanuzi kuhusu Mpango wa Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima Mjini Kilwa Masoko.
Ofisa Mafao wa NSSF, Kabonwa Kandoro akiwaandikisha
uanachama Wenyeviti na Makatibu wa vyama vya wakulima AMCOS baada ya semina
iliyofanyika Kilwa Masoko mkoani Lindi.
No comments:
Post a Comment