Mhasibu Mwandamizi wa UTT AMIS Bwana Dogo Balima (kushoto) akimkabidhi Bi. Ruth Mollel ambaye ni Mwenyekiti wa Ruth Mollel Foundation hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia watoto njiti.Kulia ni Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa UTT AMIS Bw. Mfaume Kimario akishuhudia makabidhiano hayo.
Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi Bw. Mfaume Kimario akiongea na waandishi wa habari baada ya UTT AMIS kutoa msaada kwa Ruth Mollel foundation kwa ajili ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Bi Ruth Mollel akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kupokea msaaada ya shilingi Milioni 2 kutoka UTT AMIS kwa ajili ya
kusaidia watoto njiti.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
UTT AMIS ni
kampuni inayoendesha mifuko ya uwekezaji
wa pamoja hapa nchini. Mpaka sasa inaendesha mifuko mitano ambayo ni Mfuko wa
Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko wa Watoto, Mfuko wa Kujikimu na Mfuko wa
Ukwasi yenye jumla ya thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 250.
Mifuko ya uwekezaji wa pamoja ni fursa mbadala inayowezasha watu
,vikundi,taasisi na kampuni sawa na mahitaji yao kuwekeza pesa zao kwa meneja
wa mfuko(UTT AMIS) kisha meneja huwekeza fedha hizo katika masoko ya fedha na
masoko ya mitaji kulingana na waraka wa makubaliano. Faida ipatikanayo
hugawanywa kwa wawekezaji kulingana na uwiano wa uwekezaji waliofanya katika
mfuko husika.
Mifuko yote hii
imeweza kukidhi vigezo muhimu vya
uwekezaji ambavyo ni Usalama,Ukwasi na Faida (Safety, Liquidity and Returns). Wawekezaji wote wananufaika kwa kupata faida shindani, uwekezaji mseto
hufanyika ili kupunguza hatari za uwekezaji,utalaamu wa meneja wa mifuko,unafuu
wa mkubwa wa gharama na uwazi kwani bei halisi ya vipande vya mifuko hutangazwa
kila siku za kazi.
UTT AMIS - Mshirika hakika katika uwekezaji.
No comments:
Post a Comment