Taarifa kwa vyombo vya habari
Ndugu wanahabari na Watanzania kwa ujumla sisi wana CCM wa Wilaya ya Kilombero tunawashukuru
kwa kuwepo uchaguzi wenye amani na utulivu.
Tunawapongeza wananchi wa wilaya ya Kilombero
yenye majimbo mawili ambayo ni Mlimba na Kilombero na Tanzania nzima kwa kuwa na utulivu.
Baada ya kusema hayo tunapenda sasa kutoa taarifa rasmi kwa umma kwamba sisi wanachama wa CCM
tunawaomba viongozi wetu wa CCM Wilaya kujiondoa wenyewe ndani ya siku 21 kuanzia leo 2
Novemba, 2015.
Kwamba, kama hawatafanya hivyo tutalazimika kutumia taratibu zingine za kichama
kuwaondoa.
Ingawa wapo viongozi wengine wa CCM Wilaya ya Kilombero wanaopaswa kujiondoa, ambao
tungependa waondoke mara moja ni, Abdallah Kambangwa ambaye ni Mwenyekiti CCM (W) Kilombero,
Pelegrin Kifyonga, Katibu Mwenezi CCM (W) Kilombero na Bakari Mfaume, Katibu wa CCM (W)
Kilombero.
Sababu kuu za kuwataka waondoke madarakani ni kutokana na CCM kupoteza ubunge katika majimbo
yote mawili Mlimba na Kilombero huku wao wenyewe wakionekana kama ndio sababu kuu.
Kama ilivyo
katika michezo kwamba timu inapofungwa mfululizo kocha na safu yake ya ufundi anapaswa kuachia
ngapi, tunaona ni busara kwa viongozi hao kuondoka madarakani. Dalili za kuanguka kwa chama zilianza
kuonekana wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa, lakini hakuna hatua za dhati zilizochukuliwa.
Kwa kifupi ni kwamba wilaya imepoteza madiwani; imeambulia madiwani 7 huku Chadema ikipata 9
Jimbo la Mlimba, kwa jimbo la Kilombero CCM imepata madiwani 10, Chadema 8 na CUF mmoja. Katika
mahesabu ya jumla ni kwamba halmashauri ya Kilombero sasa inakuwa chini ya Ukawa, jambo
limetuumiza sana wana CCM, kwani sababu kubwa za kuanguka pamoja na mambo mengine ni uongozi
duni wa CCM wilaya.
Kwamba baada ya kushindwa uchaguzi tuliwasiliana wana CCM karibu wilaya nzima, kata na matawi,
tumefanya utafiti na kubaini sababu za kuanguka kwa CCM, mojawapo ni harakati duni za kuimarisha
chama toka kwa viongozi wa CCM wilaya, kwa mfano hata idadi ya wanachama katika kata mbalimbali ni
ndogo ukilinganisha na uwiano wa wananchi waliopo.
Kwamba, baadhi ya viongozi wamekuwa wakiwakumbatia watia nia, huku wengine wamekuwa
wakishirikiana na wafanyabiashara ili kuwapitisha watu fulani kugombea kwa maslahi ya watu fulani
katika mazingira ambayo yanatafsiriwa na baadhi ya wana CCM kama mawasiliano tata yenye kuathiri
uhai wa chama.
Wapo baadhi ya wana CCM wameshauri tuombe kibali Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ili
tuprinti kumbukumbu za mawasiliano baina ya baadhi ya viongozi wa CCM wilaya Kilombero na baadhi
ya watu hasa watia nia/wagombea na wafanyabiashara, hata hivyo tusingependa kufika huko.
Tusingependa kuangalia ni kiasi gani cha fedha kimetumwa kwa kiongozi gani wa CCM wilaya kwa
sababu gani, tunapenda kwa hekima za viongozi wa CCM wilaya kama wakuu wa chama, wajiondoe
wenyewe hasa baada ya chama kufanya vibaya katika uchaguzi mkuu.
Tunaamini hii italinda heshima
yenu nay a chama kwa ujumla.
Kwamba mpango huu wa kuwataka waondoke madarakani ni ajenda ambayo inahusisha wana CCM
zaidi ya 1207 kutoka kata zote za wilaya ya Kilombero zikiwemo Kidatu.
Matawi na mashina yote ya CCM
yana taarifa juu ya mpango huu na baadhi ya wanachama/viongozi wa taasisi za CCM wilaya na mkoa
wanaunga mkono mpango huu wa kuwataka muondoke ili kupisha viongozi wa muda kabla ya kufanyika
uchaguzi. Majina ya baadhi ya wale wanaounga mkono mpango huu hayataandikwa kwa sababu
maalum.
Wako katika Ujenzi wa chama
Wako
Dismas Lyassa
Kiongozi wa Mpango wa Kuimarisha CCM (W) Kilombero
0688487745 na 0754498972
Kwa kufupisha tu orodha ndefu ya wana CCM wilaya ya Kilombero waliounga mkono mpango huu,
wafuatao ni baadhi yao, namba zao za uanachama au namba zao za simu:
1. Yohana Malonja Magembe AF 5635781, kata ya Kidatu, simu namba 0687470245
2.Cussy Mchola, wa Mngeta, simu namba 0786930045
3.Justin Kofiaupande Mhonda,Katibu wa CCM Kata ya Uchindile, 0784910605
4.Bilali Mwamunyi, 273647606, Kata ya Mchombe, 0688885419
5.Alfred John Sinkala, katibu tawi la Ijia, Kata ya Mchombe, AE4094367, simu0683405714
6.Ester Mfugale, Kata ya Mchombe, simu 0787534202
7.Aron Nyagawa, 831495, Kata ya Ching’anda, 0782082349
8.Boniface Mwaduma, AG 6747040, Mwenyekiti UVCCM Kata ya Igima, 0682688030
9.Mwl Kunibert Gabriel Lihambamoyo, TANU C221316 na CCM A968092, Kata ya Chisano,
0766126770
10.
Pilimini Mwinuka, Kamanda wa chama, Aa757964, Kata ya Igima, 0787000918
11.Pengo Soma, AC727026, Katibu Tawi, Mchombe, 0786314450
12.Emannuel Garugwa Izengo, AF5763516, Kata ya Namwawala, 0787351869
13.Theodos Simbakalala, kata ya Mofu, aa89813, simu 0682485864
14.Fredi Mchola, Kata ya Mchombe, 0789696322
15.Mwanaisha Mpaku, simu namba 0788452994
Hawa ni baadhi ya wanachama, kama nilivyosema orodha yao ni ndefu; wanachama kutoka kata
zote wanaunga mkono kuondolewa kwa viongozi wa CCM wilaya Kilombero
Nakala kwa
Katibu Mkuu wa CCM (T)
Katibu wa CCM (M) Morogoro
Wako katika ujenzi wa taifa
Dismas Lyassa
Kwa niaba ya wana CCM wa Wilaya ya Kilombero
0688487745
No comments:
Post a Comment