Meneja wa Kampuni ya Mitandao ya
Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Airtel Tawi la Zanzibar bwana Muhidin
Mikidadi wa kwanza kutoka kulia akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kuliani
kwake Ofisini Vuga Mjini Zanzibar.
Bwana Muhidini alifika Ofisini kwa Balozi Seif
kukabidhi mchango wa Shilingi Milioni Moja kwa ajili ya kusaidia Sherehe za
Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 52.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu wa Makamu wa Pili
Nd. Abdullah Ali Abdullah (Kitole) na Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim.
Meneja wa Kampuni ya Mitandao ya
Mawasiliano ya Simu za Mkononi ya Airtel Tawi la Zanzibar bwana Muhidin
Mikidadi akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Mchango wa
shilingi Milioni 1,000,000/- kusaidia sherehe za Mapinduzi kutimia miaka 52.
Balozi Seif Ali Iddi akimshukuru
Meneja huyo wa Airtel Tawi la Zanzibar kwa mchango mkubwa utakaosaidia huduma
za sherehe Mapinduzi katika mambo mbali mbali.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif akibadilishana mawazo na Meneja wa Tawi la Kampuni ya Mitandao ya simu za
Mkononi Zanzibar Bwana Muhidin Mikidadi. Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment