Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es
Salaam na viunga vyake, wakiwa katika ibada ya mkesha wa mwaka mpya katika Uwanja wa Uhuru. (Picha na
Francis Dande)
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi, akipongezana na mke wake wakati wa mkesha wa mwaka 2016.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi, akiwa na mke wake wakati wa mkesha wa mwaka 2016.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi, wakiwa katika mkesha wa mwaka 2016.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake wakishangilia ilipotimia saa sita kamili katika mkesha wa mwaka mpya.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake wakishangilia baada ya kutimia saa sita kamili usiku kwenye Uwanja wa Uhuru, walipokuwa wakisherehekea mwaka mpya.
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake wakishangilia baada ya kutimia saa sita kamili usiku kwenye Uwanja wa Uhuru, walipokuwa wakisherehekea mwaka mpya.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi na mkewe wakicheza kwa furaha wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, akiwa na furaha wakati wa mkesha wa mwaka 2016 kwenye Uwanja wa Uhuru.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akicheza nyimbo za injili wakati wa mkesha wa mwaka mpya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkesha wa Kuliombea Taifa (Dua maalum), Mchungaji Godfrey Mallassu akizungumza katika mkesha huo.
Brass Band ikitoa burudani wakati wa mkesha huo.
Watu mbalimbali waliohudhuria tamasha la kuliombea Taifa wakitoa sadaka.
Kwaya ikiimba.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi ambaye alimwakilisha Rais Dk. John Magufuli akitoa hotuba yake.
DJ Timber
akifanya vitu vyake wakati wa mkesha wa mwaka mpya uliofanyika kwenye Ukumbi wa
Club Bilz, Posta jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM, Tanzania
WAKATI Rais Dk. John
Magufuli akizidi kuwaomba waumini wa dini mbalimbali nchini kumuombea katika
mchakato wake wa kupambana na mafisadi, amewataka Watanzania kutumbua majipu
madogo wanayoishi nayo mitaani likiwamo la uhujumu uchumi ili taifa liweze kusonga
mbele.
Tangu Serikali ya Awamu ya Nne
iingie madarakani imekuwa ikiwachukulia hatua mbalimbali wala rushwa na wakwepa
kodi ambao walichangia serikali kupoteza mapato.
Akizungumza katika mkesha wa
kuliombea taifa pamoja na kuukaribisha mwaka 2016 jijini Dar es Salaam juzi kwa
niaba ya Rais Dk. Magufuli, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,
William Lukuvi, alisema kwa kipindi kirefu taifa limekabiliwa na vigogo
wanaouza dawa za kulevya, wakwepaji wa kodi, walaji wa fedha za maendeleo
pamoja na wizi wa dawa katika hospitali nchini.
Lukuvi alisema kuwa Watanzania
hawapaswi kumuachia mzigo huo Rais Magufuli peke yake bali wawe tayari
kukabiliana na majipu hayo kutokana na idadi kubwa ya wabadhirifu hao wanaoanzia
ngazi za chini, wakiwamo watumishi wa halmashauri ambao wanaweza kuwajibishwa
na wananchi kabla ya kumsubiri rais.
“Kazi iliyopo hivi sasa ni
kwa viongozi wa dini na Watanzania kulivalia njuga suala hili na kila mtu aweze
kuyatumbua majipu hayo ambayo yanakwamisha mafanikio ya kimaendeleo,” alisema.
Waziri huyo alisema viongozi
wa dini wanapaswa kuendelea kuliombea taifa hasa kwa wale wasiopenda maendeleo ili
waweze kubadilika, hatua itakayosaidia kuweza kupiga hatua.
Alisema ubadhirifu wa mali
za umma umechangia kuzorotesha maendeleo ya Watanzania kutokana na watu
wachache wasiokuwa waaminifu serikalini kuendekeza vitendo vya rushwa.
“Viongozi wa dini wanapaswa
kuwahubiria waumini wao kuwa wafanye kazi kwa bidii kwani hata vitabu vya dini
vinaeleza kwamba asiyefanya kazi na asile, hivyo kutokana na kauli ya ‘Hapa
Kazi Tu’ ni lazima ifanywe kwa vitendo,” alisema.
Lukuvi aliwataka Watanzania waendelee
kuwa wamoja na kumuunga mkono Rais Dk. Magufuli kutokana na hatua mbalimbali
anazozichukua dhidi ya watumishi wa umma, kukabiliana na wizi wa dawa katika
vituo vya afya na watumishi wazembe ambao hawafanyi kazi kama inavyohitajika.
Kuhusu suala la amani,
Lukuvi alibainisha kuwa inatakiwa kuendelezwa kwa ushirikiano bila kujali
itikadi za vyama na dini zao ili kutunza umoja, mshikamano na amani iliyopo ambayo
imedumu tangu taifa lipate uhuru.
“Kama yalivyo malengo ya serikali
hii ya Awamu ya Tano kwamba tutafanya kazi chini ya misingi ya haki bila
ubaguzi wa dini, rangi wala kabila, hivyo hata wananchi nao wanatakiwa
kulifanya hilo,” alisema.
No comments:
Post a Comment