SHIRIKISHO la Riadha Tanzania(RT) limeandaa mbio fupi kwa ajili ya
kuhitimisha siku 100 za rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Ikulu zitakazotimua
vumbi jumamosi hii januari 30 mwaka huu
mjini Dodoma.
Mbio hizo zimepewa jina
maalumu la Dodoma ‘hapa kazi tu’ Half Marathon ambazo zitashirikisha washiriki
mbali mbali wakiwamo waheshimiwa
wabunge,mawaziri,wanafunzi,walemavu na wanariadha wakongwe nchini.
Akizindua mbio hizo mjini Moshi
mwishoni mwa wiki zinazodhaminiwa na Kampuni ya GSM Foundation, Rais wa
shirikisho hilo, Anthony Mtaka (pichani) alisema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mbio hizo
ambazo zimeandaliwa na kuendeshwa na shirikisho hilo ni kufufua michezo hapa
nchini.
Pia alisema mbio hizo
zitatumika kwa ajili ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kutimiza siku
100 tangu aingie maradakani ambazo zitakuwa februari 14 mwaka huu.
Kwa mujibu wa rais huyo wa
RT,mbio hizo zimegawanywa katika makundi matatu ambako mbio za kwanza ni za kilomita
2.5 ambazo zitashirikisha wabunge,mawaziri,walemavu,wanafunzi ,wazee na watu
mbalimbali.
Mbio za kilomita 5 ambazo ni
za kujifurahisha zitashirikisha wakimbiaji wote na mbio za nusu marathon ambazo
zitakuwa ni mbio za ushindani washindi watapata zawadi .
Akitangaza zawadi kwa washindi,Mtaka alisema mshindi wa kwanza
kwa upande wa wanaumme na wanawake atapata zawadi ya piki piki yenye thamani ya sh,Milioni
2.8,mshindi wa pili akipata bati 100,wa tatu bati 40,mshindi wa nne akipata
sh,200,000 huku mshindi wa tano akiondoka nash,100,000.
Mshindi wa sita hadi wa kumi
watapata kifuta jasho cha sh,50,000 kila mmoja huku waziri Mkuu Majaliwa Kassim
Majaliwa ndiye atayakuwa mgeni rasmi
katika ufunguzi wa mbio hizo na atashiriki
mbio za kilomita 2.5.
Wanafunzi waatakaopenda
kushiriki mbio hizo watasajiliwa kwa sh,500,huku vwasio wanafunzi wakisajiliwa
kwa sh,1,000 na wingine ambao hawakutajwa ni kundi gani wakisajiliwa kwa
sh,5,000 na fedha hizo kwa mujibu wa Mtaka zitasaidia kambi ya wanariadha watakaoshiriki
michuano ya Olimpiki.
Uzinduzi huo pia ulitumika
kuwatambulisha wanariadha wawili ambao wamekidhi vigezo vya kushiriki michuano
ya Olimpiki itakayofanyika nchini Brazil mapema mwezi Agosti mwaka
huu ambako nchi zaidi ya 216 kutoka kila kona ya dunia zitashiriki.
Wanariadha hao ni Alphonce
Felix ambaye ana wastani wa muda wa kukimbia wa saa 2:12.01 na Said Makula
ambaye muda wake wa kukimbia ni saa 2:13.27 na watatumia mbio hizo mjini Dodoma
kama majaribio yao ya kitaifa kati ya majaribio sita ya kitaifa kabla ya kwenda
Brazil.
Julai 6 mwaka jana,Felix
alishiriki mbio za Gold Coast Marathon nchini Australia na kumaliza nafasi ya
sita huku Makula akishiriki mbio za Casablanca Marathon oktoba 25 mwaka
jana na kumaliza katika nafasi ya nne.
Imeandaliwa na Charles
Ndagulla,Rodrick Mushi na Dixon Busagaga.
No comments:
Post a Comment