Mhandisi Mohamed Millanga akiongoza
msafara wa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa
kukagua ujenzi wa jengo la tatu la abiria (TBIII).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa (katikati) akipata maelezo ya maendeleo
ya ujenzi wa TBIII kutoka kwa mhandisi Mohamed Millanga (kulia).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jengo la tatu la abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Prof. Makame Mbarawa.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
Waziri akiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman S. Suleiman (aliyenyoosha mkono) akimpa
maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa jingo la tatu la abiria, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Pro. Makame Mbarawa.
Waziri waWizara ya Ujenzi,. Uchukuzi na
Mawasiliano, Mh. Prtof Makame Mbarawa akisaini kitabu cha wageni katika jingo
la kikosi cha zimamoto cha kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA).
DAR ES SALAAM, Tanzania
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mh.Prof. Makame Mbarawa ameagiza watumishi wa Tassisi zote
zinazotoa huduma katika viwanja
vya ndege hapa nchini kuwajibika kwa
Mameneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA)
wanaosimamia viwanja ambavyo
watumishi hao wamepangiwa kufanya
kazi.
Mh. Mbarawa ametoa agizo hilo
jana wakati alipofanya ziara ya siku moja kwenye Makao Makuu ya
TAA ambapo pamoja na mambo mengine alikagua ujenzi unaondelea wa jengo la tatu la abiria
(TBIII), na kituo cha Zimamoto na
Uokoaji. Pia alitembelea mradi wa usimikaji wa vivuko vipya vya abiria (Passenger Boarding Bridges) na usimikaji wa mitambo mipya ya kufua umeme wa
dharura (Standby Generators) iliyopo
katika kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Akizungumza na menejimenti ya TAA ikiongozwa na
Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Suleiman S.
Suleiman katika Ofisi za TAA
ikiwa ni sehemu ya majumuisho ya ziara yake, Prof. Mbarawa aliwapongeza
TAA kwa kazi nzuri wanayoifanya hususan
katika uboreshaji wa muindombinu na kuhudumia wateja. Hata hivyo alisema
pamoja na sifa hiyo nzuri, kuna haja kwa TAA kuwa mdhibiti wa taasisi nyingine
zote zinazofanyakazi katika viwanja vya ndege hapa nchini kama njia ya kuepuka kuchafua sifa nzuri ya viwanja hivyo
na nchi kwa ujumla.
“ Pamoja na kazi nzuri mnayoifanya,nadhani wakati umefika sasa kwa taasisi zote
zinazotoa huduma katika viwanja vya ndege hapa nchini ziwe chini ya TAA”, alisema
Prof. Mbarawa huku akisisitiza
umuhimu wa taasisi hizo kufanya
kazi kwa kushirikiana kama timu moja.
“Nyinyi ndio kioo katika jamii yetu, taasisi
nyingine mfano uhamiaji wakachelewa kugonga mhuri kwenye hati za kusafiria,
watu hawatambui kama ndio wao waliochelewesha na lawama watawatupia nyinyi,”
alisisitiza Mh. Mbarawa na kuongeza kwamba anafanya utaratibu wa kuwasiliana na
Wizara zote zinazohusiana na taasisi
hizo ili kupanga utaratibu muafaka.
Mbali na idara ya uhamiaji, taasisi nyingine zinazotoa huduma kwenye
viwanja vya ndege ni pamoja na Idara ya maliasili, afya, kilimo, mifugo, madini, polisi na kitengo cha kuzuia madawa ya
kulevya.
Mh. Mbarawa pia
ameiagiza TAA kubuni mikakati
ya kuongeza ukusanyaji wa mapato zaidi ili iweze kujiendesha na pia
ihakikishe kuwa inaepukana na matumizi
yasiyo ya lazima. Aliitaka watumishi wa TAA kuzingatia uadilifu na weledi katika utendaji
wao wa kazi na kuhudumia wateja
ikizingatiwa kuwa viwanja vya ndege ni kioo cha nchi.
“Nisingependa taarifa za matukio
mbalimbali yanayotokea kwenye viwanja niyasikie au kuyaona kwenye vyombo vya
habari wakati mimi mwenyewe sijui, hivyo tujenge utamaduni wa kuwa waadilifu na
tufanye kazi kwa kuzingatia weledi, tuepukane na matukio ya hovyo,” alisisitiza
Mh. Mbarawa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TAA,
Mhandisi S.S.Suleiman alimhakikishia Waziri Mbarawa kutekeleza maagizo yake,
likiwemo la kubuni mbinu mpya za mapato, na hata kuweka utaratibu wa kumpatia
taarifa mbalimbali zinazotokea kwenye viwanja kabla hazijapelekwa sehemu
nyingine yeyote, kwa ajili ya utekelezaji na kujenga uhusiano mzuri baina ya
mamlaka na wizara kwa ujumla.
“Kuhusu mapato tunauhakika wakati
wa jengo la tatu la abiria likifunguliwa yataongezeka, lakini tunaahidi kubuni
mbinu nyingi zaidi, ili tuwe na vyanzo
vya uhakika vya mapato,” alisema Mhandishi Suleiman. Alisema kukamilika kwa jengo
hilo kutaongeza idadi ya abiria watakaosafiri na ndege za ukubwa mbalimbali
ikiwemo 380 Airbus yenye uwezo wa kubeba abiria 300.
Awali Mh. Mbarawa alipotembelea
ofisi za zimamoto zilizopo JNIA, alielezwa wanakabiliwa na changamoto ya uhaba
wa vifaa na hususan magari ya zimamoto
ambayo mbali na kuhudumia viwanja vya ndege, wakati mwingine kulazimika pia kusaidia jamii endapo nyumba zao zinakumbwa na majanga
ya moto.
Imetolewa na kitengo cha Habari na
Mahusiano na Sheria TAA.
No comments:
Post a Comment