Katika kuadhimisha miaka 17 ya kumbukuzi ya mwaasisi wa chuo
kikuu cha kumbukumbu ya Hubert kairuki kuanzia tarehe 4
hadi 6 Feb ambayo itakuwa ni siku ya kilele.Mh Dr Salmin
Ahmed Salim ambaye pia ndio mkuu wa chuo hicho atazindua jengo la
utafiti na mafunzo ya Uyoga lililopo huko Boko katika
eneo la chuo hicho.
Sambamba
na uzinduzi huo pia shughuli nyingine katika kumbukizo
hizo itakuwa ni pamoja na muhadhara kuhusu Uyoga utakaotolewa na
Profesa Keto Mshigeni ambaye ndiye makamu mkuu wa
chuo hicho na mwanasayansi aliyebobea katika tafiti za uyoga.
Pia
hospital ya Kairuki it ataendesha zoezi maalum la upimaji na matibabu ya
macho bila ya malipo kwa siku mbili mfululizo.
Pia
patakuwepo matembezi ya hiara kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya
saratani ya kizazi.
Aidha wanafunzi wa zamani wa chuo hicho
waliopo Mwanza na mikoa ya kanda ya ziwa wataadhimisha
kumbukizo hizo kwa kufanya zoezi la kupima afya
bure kwa wakazi wa huko.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert Kairuki yatakayofanyika kuanzia Februari 4. Kushoto ni Ofisa
Habari wa chuo hicho, Abraham Mwalugeni.
Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Afya na Elimu la
Kairuki (KHEN), Dk. Muganyizi Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya 17 ya kumbukumbu ya Prof. Hubert
Kairuki yatakayofanyika Februari 4. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu
ya Kairuki, Prof. Keto Mshigeni na Ofisa Habari wa chuo hicho, Abraham
Mwalugeni.
No comments:
Post a Comment