Na Mwandishi Wetu
Shule ya sekondari ya
Shimbwe iliyopo wilaya ya Moshi vijijini,Imenufaika na msaada wa mashine yenye
uwezo wa kufanya kazi zaidi ya tatu ikiwemo kudurusu karatasi kupitia
mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom Tanzania”Vodacom Foundation”.
Msaada wa mashine hiyo
(Photocopier) yenye thamani ya zaidi ya sh Mil 12 ni sehemu ya msaada wa vifaa
mbalimbali ambavyo kampuni hiyo kupitia mradi wa “Pamoja na Vodacom” imekabidhi
shuleni hapo zikiwemo Kompyuta mpakato 30.
Mbali na msaada wa
Kompyuta na Mashine hiyo kampuni hiyo pia ilitoa wataalamu kutoka shirika
lisilo la kiserikali la Learning in Sync kwa ajili ya kuweka program
maalumu katika kmpyuta za kufundishia na kujifunzia .
Mkuu wa Vodacom Tanzania
Kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis alisema kutolewa kwa mashine hiyo ni
muendelezo wa msaada ambao Vodacom kupittia mradi wa Pamoja na Vodacom
imeendelea kutoa kwa nchi nzima.
“Huu ni muendelezo wa
msaada ulitolewa awali ,Kampuni ya Vodacom tunarudisha sehemu ya faida kwa
wananchi na wateja wetu,pamoja na hayo ni kusaidia wadogo zetu kuingia katika
digitali wakiwa na umri mdogo na kuwaandaa na maisha ya baadae,”alisema
Tzamburakis.
Alisema Mashine hiyo ya
kisasa itasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili shule hiyo
hususani katika maandalizi ya mitihani pamoja na machapisho mengine ambayo
shule ili lazimika kuingia gharama kubwa kuchapisha.
Katika kuhakikisha walimu
wa shule hiyo wanaweza kutumia vyema mashine hiyo Tzamburakis alisema ofisi ya
Vodacom kanda ya Kaskazini itatoa mtaalamu kwa ajili ya kufundisha namna ya
kuitumia.
“Ofisi ya kanda ya
Vodacom ina wataalamu wa IT ambao watasaidia katika kutoa mafunzo kwa walimu ya
namna ya kutumia mashine hizi na tutaweka utaratibu wa kufika mara moja kwa
mwezi katika shule hii ili waweze kubadilishana uzoefu na walimu wa masomo
hayo.”alisema Tzamburakis.
Kwa upande wake mkuu wa
shule ya sekondari Shimbwe,Jacob Costantine aliishikuru kampuni ya Vodacom kwa
msaada huo huku akieleza changamoto zilizoikabili shule hiyo ikiwemo ya kuchapisha
mitihani kwa gharama kubwa .
“Tumepewa mashine ya
Photocopy ikiwa ni ahadi ya mgeni rasmi kutoka Vodacom baada ya kumueleza kuwa
tumekuwa tukitumia gharama kubwa hasa kipindi cha mitihani ,kuchapisha mitihani
yetu ya mihula na ile ya mwisho wa mwaka”alisema Costantine.
Alisema kupatikana kwa
mashine hiyo ,sasa shule itakuwa na uwezo mkubwa wa kuchapisha machapisho
mbalimbali vikiwemo vitabu ambavyo upatikanaji wake umekuwa mgumu kwa ajili ya
wanafunzi hao kujifunzia.
Mkuu huyo wa shule
alisema wamekuwa wakitumia zaidi ya shilingi Milioni nne kwa ajili ya
maandalizi ya mitihani shulebi hapo na kwamba kwa sasa adha ya kuandika ubaoni
mitihani ya majaribio itatoweka.
No comments:
Post a Comment