Kilio cha Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), upande wa Zanzibar kimesikilizwa kilio chao cha kutaka uswa wa kijinsia katika viongozi wa juu wa Serikali na katika vyombo vya kutoa mamuzi pale Bara za wawakilishi lilipomchagua Mgeni Hassani Juma (pichani), kuwa Naibu Spika wa Baraza hilo.
Akitoa matoke hayo Katibu wa Baraza hilo, Yahya Khamis Hamad alisema mgombea huyo aliyekuwa pekee kutoka na Baraza kukosa mwakilishi kutoka upinzani alipata kura 73 kati 74na moja kumkataa .
Akitoa shukrani Mgeni alisema kuchaguliwa kwake kumempa imani na vipi anavyokubalika na kutoa ahadi ya kutenda kazi hiyo kwa misingi ya haki.
“Ushirikiano wenu ndio nguvu yangu katika kufanyakazi hii yetu sote kwa siyo yangu mimi tuu” alisema Mgeni.
Sambamba na hilo Baraza hilo pia lilichagu wenyeviti wawili kwa kulingana Jensia zote ambao ni Sheha Hamad Matari na Bi Riziki Pembe Juma ambao wote walichaguliwa kwa kura 73 kila mmoja.
Wenye viti hao waliaahidi wajumbe kufanya kazi kwa bidii na juhudi za hali ya juu kwa ajili ya maendeleo ya baraza hilo na taifa kwa ujumala.
Baada ya kukamilisha shughuli hiyo Baraza la Wawakilishi linasubiri kwa hamu siku ya Jumatano tarehe 5 ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein anatarajiwa kulihutubia.
"Tunatarajia Rais wetu atalihutubia Baraza letu siku ya Jumatano katika kikao cha asubuhi majira ya nne asubuhi” alfahamisha Spika wa Baraza hilo Zubeir Ali Maulid.
Mara baada ya kutolewa ghotba hiyo wajumbe watapata muda wa muijadili kama ilivyotaratibu za mabunge yote ulimwenguni.
No comments:
Post a Comment