HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 10, 2016

NSSF: NSSF YAZIDI KUJIZOLEA WANACHAMA WA HIARI

Wananchi wa eneo la Banana jijini Dar es Salaam wakiwa katika foleni ya kujiandikisha katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF.

Na Mwandishi Wetu

Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), bado linaendelea na zoezi lake maalum la kukusanya michango kutoka kwa waajiri  na wapangaji wenye madeni sugu kabla hawajawachukilia hatua za kisheria.

Sambamba na zoezi hilo, shirika linafanya kampeni kabambe kupitia kliniki za huduma (customer care clinics) za kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na masuala ya shirika, mafao lukuki yatolewayo na faida za kujiunga kwa hiari chini ya mpango mahsusi wa ‘hiari scheme’ unaoshughulikia wanachama wa hiari.

Taarifa iliyotolewa na NSSF imesema kuwa zoezi hilo lilianza Mei 2 na Mkoa wa Temeke ambapo vituo viliwekwa katika maeneo ya Mwembeyanga, Mbagala na Banana kwa ajili  ya kutoa elimu na kusajili wanachama wapya ambapo jumla ya wanachama  512 waliandikiswa. 

Kwa wilaya ya Kinondoni vituo viliwekwa Tegeta ambapo wanachama 196 waliandikishwa na Mwenge wanachama 192 kwa siku.

Shirika linatoa rai kwa wananchi kuitumia fursa hii ipasavyo ili kuweza kunufaika na mafao bora yatolewayo.vile vile linawasisitizia waajiri wote kuandikisha na kuwachangia wanachama wao kama inavyostahili pamoja na elimu kwa umma, Shirika linatoa huduma ya kupokea malalamiko na maswali ili kuweza kutoa huduma bora zaidi katika kliniki za huduma (customer care clinics) Shirika linawakumbusha pia wale wanachama wote wataoshindwa kufika kwenye kliniki hizi za huduma wapige simu  ya bure 0800 75 6773 kwa huduma zaidi na kwa kupokea malalamiko au watembelee ofisi zetu zilizopo karibu nao.



Zoezi hilo linaendelea Mei 9 katika maeneo ya Mbezi ya Kimara ambapo Mei 10 wananchi wanaoishi jirani na kituo cha basi cha Makumbusho watapata fursa ya kujiandikisha na wakazi wa Ilala Sokoni Mei 11, Mei 12 watakuwa Buguruni Sokoni, mei 13 Kariakoo Sokoni kwaajili ya kuelimisha na kusajili kwa hiari. 

Baada ya hapo zoezi litaendelea mikoani likianza na mkoa wa Arusha likifuatiliwa na mkoa wa mwanza.

No comments:

Post a Comment

Pages