Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akionyeshwa barabara zinazopishana juu
na chini na Meneja wa Ujenzi wa Daraja la Nyerere Mhandisi Karim Mataka wakati alipofanya ziara katika daraja hilo
jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akikagua Daraja la Nyerere wakati
alipofanya ziara katika daraja hilo jijini Dar es Salaam.
Mhandisi Karim Mataka akitoa ufafanuzi kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete. kuhusu Daraja la Nyerere.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika ziara ya kutembelea Daraja la Nyerere.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa na mkewe wakitembea katika
Daraja la Nyerere wakati walipotembelea daraja hilo jijini Dar es Salaam.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akishangaa daraja la Nyerere. Kulia ni Mama Salma Kikwete.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa amefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pamoja na viongozi wengine. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiwa akipata maelezo kuhusu mfumo wa ulipaji wa tozo katika daraja la Nyerere. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na katikati ni Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula.
Mfanyakazi wa NSSF akimkatia tiketi Rais mstaafu wakati alipofanya ziara katika daraja la Nyerere.
Maofisa wa NSSF.
Mkutano ukiendelea.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga akizungumza wakati Rais mstaafu Jkaya Kikwete alipofanya ziara katika Daraja la Nyerere.
Barabara za chini za kuingia Darajani.
Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mhandisi Karim Mataka akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Barabara za chini zinazoingia katika daraja la Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia) akiangalia Barabara za chini zinazoingia katika daraja la Nyerere. Kushoti ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema.
Ofisa Mkuu Mwandamizi Idara ya Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Salim Kimaro (katikati) akiwa na maofisa wa NSSF wakati wa ziara ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete katika daraja la Nyerere.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati Rais mstaafu Jkaya Kikwete alipofanya ziara katika Daraja la Nyerere.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akizungumza mara baada ya kufanya ziara katika Daraja la Nyerere jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga akitangaza tozo za vyombo vya usafiri vitakavyotumia Daraja la Nyerere.
Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacoub Kidula akizungumza kuhusu namna NSSF itakavyondesha daraja hilo.
No comments:
Post a Comment