HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 11, 2016

WARAMI WAMPONGEZA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUWATETEA WANYONGE, WASEMA ANAPIGWA VITA NDANI YA BUNGE NA NJE YA BUNGE

12
John Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka WARAMI akizungumza na waandishi wa habari Kwenye Hoteli ya Tamarin Mwenge jijini Dar es salaam kuhusu Sakata la Sukari ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa jinsi anavyothubutu kuwatetea watanzania waliowanyonge katika masuala mbalimbali na hasa katika suala zima la uhaba wa sukari.

Kuna tani nyingi za sukari zimekamatwa katika msako maalum ambao Rais aliamrisha vyombo vya dola kufuatilia wafanyabiashara wasio waaminifu walioficha sukari, baada ya zoezi hilo kuanza sukari nyingi imeendelea kukamatwa maeneo mbalimbali nchini ikiwa imefichwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.

WARAMI inapongeza jitihada zote za dhati anazozifanya Rais Magufuli na Serikali yake za kuhakikisha watanzania wanaishi kwenye usawa, lakini pamoja na hayo wanapendekeza mambo kadhaa yafanyika na jeshi la polisi.

Mratibu huyo wa Taasisi ya WARAMI amelitaka jeshi la polisi kutoa taarifa rasmi juu ya wafanyabiashara wanaotamba barabarani kuwa wameliweka jeshi hilo mfukoni kwamba hakuna wa kuwafanya lolote katika nchi hii.

Taasisi za kiserikali zifafanue juu ya tabia hii ya wafanyabiashara kutumia picha za viongozi kwa maslahi yao kama, ni haki ama si haki.

Kiongozi huyo wa WARAMI akaongeza kwamba hivi sasa Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli anayo vita kubwa kutokana na kazi anayoifanya ya kuwatetea watanzania waliowanyonge anayo vita ndani ya bunge na nje ya Bunge.

Kutokana Na Hoja Ambazo Zimekuwa Zikitolewa Na Baadhi Ya Wabunge Zikikosoa Utendaji Wa Rais, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakifaidika na baadhi ya mambo hivyo wasingependa mabadiliko ya kumkomboa mwananchi wa kawaida.

No comments:

Post a Comment

Pages