HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 27, 2016

BENKI YA CRDB TAWI LA GEITA YATOA MSAADA WA MADAWATI

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mariam Seleche (kushoto), akipokea msaa wa madawati 40 kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB, Tawi la Geita, Amin Mwakang'ata, ili kufanikisha kampeni ya kumaliza tatizo la madawati mashuleni iliyoanzishwa na Rais Dk. John Magufuli. (Na Mpiga Picha Wetu)
 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mariam Seleche (kulia), akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Cripin Mathew Luanda, madawati 40 ambayo yametolewa na Benki ya CRDB, yenye thamani ya Sh, 2,500,000. 
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mariam Seleche (kulia), (kulia), akikabidhi madawati 40 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Chalya Julius yaliyotolewa na Benki ya CRDB. 
 Picha No 2 na 3 Meneja wa Tawi la Crdb Bank Geita akitoa maelezo machache kabla ya kukabidhi madawati kwa mkuu wa wilaya Sengerema
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Cripin Mathew Luanda, akizungumza katika hafla ya kupokea msaada wa madawati 40 ambayo yametolewa na Benki ya CRDB, yenye thamani ya Sh, 2,500,000. 
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Chalya Julius akitoa shukran baada ya kupokea msaada wa madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB. 
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mariam Seleche akiipongeza benki ya CRDB katika  kuboresha sekta ya elimu.  

NA MWANDISHI WETU, GEITA

BENKI ya CRDB tawi la Geita limetoa msaada wa madawati katika kukabiliana na upungufu ili kuboresha sekta ya elimu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo Meneja wa CRDB tawi la Geita, Amin, alisema kwamba wameendelea kuitikia wito wa Rais John Magufuli na kuona umuhimu wa sekta ya elimu.

Alisema kwamba wametoa msaada wa madawati 81 yenye thamini ya Sh. milioni tano katika halmashauri mbili za Wilaya ya Sengerema.

“Mkurugenzi wetu wa benki ya CRDB alitoa Sh milioni 200 kwa jiji la Dar es Salaam na kutenga Sh. milioni 80 kwa ajili ya Halmashauri ambazo benki yetu inashirikiana nazo kwa ukaribu Wilaya yetu imeweza kupata mchango wetu na hii ni kutokana na mahusiano ya karibu kati ya Halmashauri za Wilaya ya Sengerema na CRDB,”alisema.

Mwakang’ata alisema kwamba madawati hayo yatagawanywa makundi mawili ambapo halmashauri ya Sengerema itapewa 41 na Buchosa 40.

Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mariam Seleche, aliipongeza CRDB kwa namna ambavyo wamekuwa mstari wa mbele katika kutatua matatizo na upungufu unaojitokeza katika sekta ya elimu.

Aidha aliiomba CRDB kuendelea kushirikiana na Wilaya hiyo katika masuala mengine ya kimaendeleo na kueleza kwamba upungufu wa madawati ni janga ambalo kila kada inapaswa kushirikiana ili kulitatua.

Alisema ushirikiano huo wa wananchi, taasisi na wadau mbalimbali utaongeza mafanikio na  matokeo mazuri katika elimu.

No comments:

Post a Comment

Pages