HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 12, 2016

DC WA LONGIDO DANIEL CHONGOLO AKAGUA VYANZO VYA MAJI KUPAPAMBANA NA UHABA WA MAJI WILAYANI HUMO


Mkuu wa Wilaya ya Longido,Mh.Daniel Chongolo (pili kulia) akipata maelezo mafupi kuhusiana na moja ya chanzo cha maji ndani ya wilaya hiyo kutoka kwa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Longido,Mhandisi Musiba.DC Chongolo akifafanua jambo kwa Injinia Musiba mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo,mara baada ya kufanya ziara fupi ya kutembelea vyanzo vya maji vinavyopatikana ndani ya Wilaya hiyo katika suala zima la kuanza kuchukua hatua madhubuti ya kupapambana changamoto kubwa ya uhaba wa maji ndani ya wilaya hiyo.
DC Mh.Daniel Chongolo (pili kulia) akielekezwa jambo kwa umakini kutoka kwa Injinia Musiba,mara baada ya kuvitembelea vyanzo mbalimbali vya maji vilivyomo katika wilaya ya Longido.

DC Chongolo akiwa na kamati ya ulinzi na Usalama wakikatiza kukagua maeneo mbalimbali yenye vyanzo vya maji,katika suala zima la kupambana na uhaba wa maji uliopo katika wilaya ya Longido,ambayo imeelezwa kuwa ndio changamoto kubwa wilayani humo.

No comments:

Post a Comment

Pages