HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2016

KAMPUNI YA UR YATOA MSAADA WA MILIONI 15 KWA AJILI YA KUKUNULIA MADAWATI ZANZIBAR

Na Talib Ussi, Zanzibar

Mkurugenzi wa Kampuni ya UR, Salum Mussa Omar ametoa jumla ya Tsh 15 milioni kwa ajili ya mchango wa Madawati katika  Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ambao unakabiliwa na upungufu wa madawati 35,000.
Akizungumza na  waandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa huo Ayoub Muhammed mahmoud alisema upungufu huo  umepelea wanafunzi wengi Mashuleni kukaa chini sakafuni.

“tatizo hili ili tuweze kuliondoa basi lazima tupate madawati 35 alfu kwa mjini na maeneo mengine 15 alfu” alielezea Mahmoud.
Alisema wamegundua kukosekana  kwa vikalio katika shule nyingi mjini hapa unaoneka kuwa chanzo chengine cha kushuka kiwango cha elimu.

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa huyo alieleza kuwa licha ya upungufu huo wa madawati bado sekta ya Elimu inakabiliwa na changamoto nyengine kubwa ikiwemo uchache wa Majengo.

“Kwa mfano huu mkoa wetuu tuu  pekee unaupungufu wa vyumba vya madarasa 144 hali ambayo imepelea darasa moja kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi”aliesema Mkuu huyo wa Mkoa wa Mjini Magharbi.

alieleza kuwa mkoa wake una  shule  103 ambazo ni kidogo sana ukilinganisha nan idadi ya wanafunzi ambao wanasoma katika eneo hilo.

Mapema Mkurugenzi wa kampuni ya UR alieleza kuwa ametoa mchango huo kutokana kuwa  elimu ndio mtaji wa kuendeleza Taifa ndio na kampuni yake ikaona ni vyema kutoa mchango huo.

“kama tunataka taifa imara na elimu bora ni vyema kuwekeza katika elimu ili wanafunzi wasome bila ya ghofu” alisema Salum Mussa Omar ambaye ni mkurugenzi wa UR kampani.
Kama ilivyo kwa Tanzania bara na Rais wa Zanzibar  Ali Muhammed Shein alitoa ombi la raia wema kujitokeza kuchangia madwati kutokana upungu uliopo.

No comments:

Post a Comment

Pages