HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 25, 2016

Makongoro Nyerere anusurika ajalini akitokea Dodoma

NA GRACE MACHA, MANYARA

MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki, (EALA), Makongoro Nyerere, amenusurika kufa baada ya gari alilokuwa akiliendesha kupata ajali wakati  akitokea kwenye mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) mkoani Dodoma.

Mkutano huo wa CCM pamoja na mambo mengine ulimchangua Rais, John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Taifa akipokea kijiti kwa mtangulizi wake Rais, Jakaya Kikwete.

Ajali iliyo iliyokea juzi majira ya saa moja usiku kwenye eneo la Katanini nje kidogo ya mji wa Babati baada ya gari hilo aina ya Toyota Land Cruizer VX V8  kugonga na kuua ng'ombe saba na kondoo waliokuwa wakivuka barabara.

Makongoro ambaye ni Mwenyekiti Mstaafu huyo wa CCM, mkoani Mara na alijitokeza kuwania kuteuliwa na CCM kuwa mgombea wake kwenye uchaguzi uliopita na jina lake kuenguliwa kwenye kamati ya maadili akiongea  na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu alisema kuwa kwenye gari hiyo alikuwa peke yake na hakuumia mahali popote.

"Namshukuru Mungu nimetoka salama, leo nilikuwa namalizia mazungumzo na polisi hapa Babati sasa naondoka kuelekea Arusha," alisema Makongoro.

Kamanda wa polisi mkoani Manyara, Frances Massawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyolihusisha gari hilo lenye namba za usajili, TCD 398 EAC ambapo alisema kuwa litafanyiwa ukaguzi jijini Arusha.

Alisema ukaguzi wa gari hilo haukufanyika Babati badala yake shughuli hiyo itafanyikia jijini Arusha kwa kile alichodai kuwa baada ya ajali hiyo kutokea kulipatikana gari lenye uwezo wa kulibeba ambalo lililipeleka moja kwa moja mpaka jijini Arusha.

Kamanda Massawe alisema Makongoro jana alikutana na mmiliki wa mifugo hiyo, Mathayo Qelwe, mkazi wa kijiji cha Nakwa kata ya Bagara ambapo walifanya mazungumzo na kukubaliana ndipo akaondoka.

Hata hivyo hakuweka wazi walichokubaliana huku akieleza kuwa kijana aliyekuwa akichunga  ng'ombe hao, Willium German, hakuumia kwenye tukio hilo kwani alikimbia mara baada ya kuona ng'ombe hao wameingia barabarani na kugongwa.

No comments:

Post a Comment

Pages