Mkufunzi
klabu ya Hamilton Aquatics, Katy Morris akiwaonyesha waogeleaji chipukizi jinsi
gani ya kuanza kuogelea kwa staili ya backstroke.
Waogeleaji chipukizi chini ya miaka minne wakishiriki katika mafunzo hayo kwa
vitendo kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya DIA yaliyoandaliwa na
klabu ya Dar Swim Club chini ya ukufunzi kutoka klabu bingwa ya mchezo huo
nchini Dubai, Hamilton Aquatics.Kocha Nebojsa Durkin (wa pili kulia) akiwaelekeza makocha wa Dar Swim Club mbinu mbalimbali za kisasa za kuogelea
Na Mwandishi Wetu
Wakufunzi wa
kimataifa wa mchezo wa kuogelea wa klabu
bingwa ya Mashariki ya Kati (Middle East) ijulikanayo kwa jina la Hamilton
Aquatics ya Dubai, Nebojsa Durkin ma
Katy Morris wamesema kuwa Tanzania inaweza
kupata sifa kubwa katika michezo duniani kupitia mchezo wa kuogelea.
Wakufunzi hao
walisema hayo katika semina inayoendelea ya mchezo huo kwa waogeleaji na
makocha wa klabu marufu ya Dar Swim Club (DSC).
Durkin alisema
kuwa amefuraishwa na vipaji vya mchezo huo kutoka kwa waogeleaji wa DSC na
anaamini kuwa siku moja, Tanzania itatoa bingwa wa dunia kupitia mchezo huo.
“Nimefurahi
kuona kuwa mchezo una mwamko sana na wachezaji wanaupenda, pia Tanzania ina
makocha wazuri wenye elimu ya kutosha, naamini kama juhudi hizi zitaendelezwa, nchi itapata wawakilishi wazuri katika
mashindano ya kimataifa na kuweza hata kutwaa ubingwa wa Dunia,” alisema Durkin
ambaye ni raia wa Serbia.Alifafanua kuwa
amefuraishwa na waogoeleaji chipukizi ambao umri wao ni chini ya miaka minne.
“Nimevutiwa kuona hata Tanzania hasa klabu ya
DSC ina waogeleaji watoto ambao wanaupenda mchezo, hii imenivutia sana, hapa
utapata wachezaji ambao wataupendea mchezo kuanzia utotoni na huu ndiyo mwamko
ambao utaleta matunda katika mchezo,” alisema.
Kwa upande
wake, Katy ambaye ni mwanadada alisema kuwa wadau wa mchezo huo wanatakiwa
kusaidia kufikia malengo hayo kwani bila uwekezaji mkubwa, bado mchezo utakuwa
chini kutokana na ukosefu wa vifaa mbalimbali vya kisasa.
Katy alisema
kuwa DSC imeonyesha nia ya kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa na kuomba
wadau waunge mkoni. Mafunzo hayo yamedhaminiwa na kampuni za Alios Finance Tanzania,
Europcar, DSC, DIA na kampuni ya utafiti
na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom.
Katibu Mkuu
wa DSC, Inviolata Itatiro amesema kuwa lengo lao ni kuona Tanzania inafanya
vizuri katika mchezo huo kimataifa. Alisema kuwa DSC imeamua kupambana katika
kuleta maendeleo ya mchezo wa kuogelea hapa nchini.
“Tunahitaji
sapoti katika mchezo huu, lengo ni kuona waogeleaji wanapata maendeleo makubwa
kwa kufikia viwango, nawaopongeza wadhamini Alios Finance Tanzania, Europcar,
DSC, DIA na kampuni ya utafiti na uchimbaji wa mafuta ya Maurel & Prom kwa
kutuunga mkono, gharama za kuwaleta walimu kutoka nje ni kubwa sana,” alisema
Inviolata.





No comments:
Post a Comment