Marehemu Joseph Senga enzi za uhai wake. Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe apumzike kwa amani.
Waziri Mkuu
mstaafu, Edward Lowassa (kushoto), akiwaongoza wahariri, waandishi wa habari na
wakazi wa Jiji la Dar es Salaam leo kuaga mwili wa aliyekuwa mpigapicha wa Gazeti
la Tanzania Daima marehemu, Joseph Senga nyumbani kwake Sinza. (Picha zote na
Francis Dande)
Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akimpa pole Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Theophil Makunga katika viwanja vya TP Sinza, ambapo mwili wa Mpigapicha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima uliagwa jana ambapoJulai 31, kabla ya kusafirishwa kuelekea mkoani Mwanza kwa mazishi yatakayofanyika Agosti Mosi kijijini kwao Shushu Kwimba.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel akimpa pole Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena.
Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (kushoto), akiteta jambo na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa. Katikati ni kada wa Chadema, Khamis Mgeja.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa salamu za Serikali kwa familia ya marehemu, Joseph Senga.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu, Joseph Senga.
Baadhi ya wapigapicha wakibeba jeneza lenye mwili wa Joseph Senga wakati wakiupeleka kwenye gari kwa ajili ya safari ya kwenda Mwanza.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Free Media wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya jeneza la aliyekuwa mfanyakazi mwenzao.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Joseph Senga.
Mjane wa marehemu, Winfrida Senga (wa nne kulia), akiwa na baadhi ya wanafamilia wakiwemo watoto wa marehemu na mdogo wa marehemu (kulia).
Mpigapicha wa Gazeti la Mtanzania, Deus Mhagale akiangua kilio baada ya kuaga mwili wa marehemu Joseph Senga.
No comments:
Post a Comment