Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa
wakilisindikiza gari lililombeba mtuhumiwa kwa lengo la kuzuia wanahabari
wasipate picha.
Baadhi ya
askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa wakiwa wamemzingira mtuhumiwa wa kesi
ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Chanel
10 mkoani Iringa, Daudi Mwangosi,Pasificus Simon asipigwe picha na waandishi wa
habari wakati akirudishwa mahabusu. (Picha na Denis Mlowe)
NA
DENIS MLOWE, IRINGA.
MAHAKAMA
Kanda ya Iringa imepanga kutoa hukumu ya kesi ya mauaji ya aliyekuwa mwandishi
wa habari wa kituo cha televisheni cha Chanel 10 mkoani Iringa Daudi Mwangosi,
Julai 27 mwaka huu baada ya kumkuta na hatia ya kuua bila ya kukusudia mtuhumiwa
Pasificus Simon.
Jaji
wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa anayesikiliza kesi hiyo inayomkabili askari
polisi, Pasificus Simon, anayetuhumiwa kufanya mauji hayo, Dk. Paulo Kihwelo,
aliyasema hayo jana mara baada ya kutoa utetezi wa pande zote na maoni ya wazee
wa baraza na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 27 mwaka huu.
Jaji
Kihwelo alisema katika kesi hiyo, mtuhumiwa anadaiwa kuwa, Septemba 2, 2012
alimuua Mwangosi bila kukusudia hivyo hukumu ya kesi hiyo itafanyika mahakamani
hapo kuanzia saa nne kamili asubuhi.
Kihwelo
alisema kuwa mtuhumiwa aliweza kuepuka ushahidi mwingine uliotolewa na
mashahidi wa upande wa mashitaka lakini upande wa ushahidi aliotoa na kukiri
kuua mbele ya mlinzi wa amani umemtia hatiani na mahakama hiyo kumkuta na hatia
ya kuua bila kukusudia ambapo hukumu itatolewa siku hiyo.
Alisema
mwenye jukumu la kuthibitisha kosa kwa mtuhumiwa ni upande wa mashtaka ambao
unatakiwa uthibitishe bila kuacha shaka yoyote kuwa alifanya hivyo na si upande
wa mtuhumiwa kuthibitisha kuwa mtuhumiwa hajatenda kosa.
Jaji
Kihwelo alitaja vielelezo ambavyo vilipingwa mahakamani hapo na kuifanya
mahakama kuwa na mashaka na ushahidi ulioletwa na upande wa Jamhuri kuwa ni
ramani ya tukio, taarifa ya uchunguzi ya kifo cha marehemu na kukutwa na hatia
katika ushahidi wa ungamo la mtuhumiwa kwa mlinzi wa amani na kitabu cha
kuchukilia silaha FFU cha Iringa.
Kwa
upande wake wakili wa Jamhuri, Adoph Maganda alisema kwa kuwa mahakama imemkuta
hatiani mtuhumiwa ameitaka mahakama hiyo kumfunga kifungo cha maisha mtuhumiwa
kwa kupitia kifungu cha 198 cha adhabu za kuua bila kukusudia mtuhumiwa Pasificus
Simon.
Akizungumza
kwa niaba ya mtuhumiwa, wakili mtetezi wa Pasificus Simon, Lwezaula Kaijage
alisema kuwa kwa kuwa mahakama imemkuta na hatia ya kuua bila kukusudia
ameiomba mahakama hiyo kutambua kuwa mtuhumiwa bado ni kijana anayetegemewa na
ndugu na familia yake na kuiomba kumwachia huru mtuhumiwa.
“
Kwa kuwa mtuhumiwa aliua bila kukusudia na amekwisha tumia miaka 4 mahabusu naiomba mahakama yako tukufu kumwachia huru
mtuhumiwa kwa kuwa bado kijana na familia yake inamtegemea na ana mtoto mdogo ambaye anahitaji malezi na matunzo
kutoka kwa baba” alisema
Katika hali iliyozoeleka na kama tabia kwa jeshi la
polisi mkoa wa Iringa kuwepo ndani na nje ya mahakama zaidi ya raia ya kawaida
na kuwazuia wanahabari kufanya kazi zao hali hiyo iliendelea tena siku ya jana
kwa wanahabari mbalimbali kunyasisika hadi kutishiwa kupigwa vibao kwa lengo la
kuzuia kupiga picha mtuhumiwa.
Aidha hali ndani ya mahakamani hapo ilikuwa ya
kushangaza kwa kesi kuendelea kwa mmoja wa askari ambaye ana nyota moja kwenda
katika kizimba kuzungumza na mtuhumiwa bila maelezo ya jaji na kumwacha Jaji
Kihwelo akimwangalia kwa mshangao askari huyo.
Aidha askari hao walishindwa kuchukua hatua kwa
askari wao kupatikana na kosa la kupiga kelele kwa simu zao lakini waliwatoa tu
nje tofauti ambapo mwandishi wa gazeti la Habari Leo na mwenyekiti IPC
alipozuiliwa kupiga picha kabla mahakama kuanza.
Naye Rais wa shirikisho la vyama vya waandishi wa habari
nchini (UTPC) Deo Nsokolo alisema ameshangazwa na jeshi la polisi kuingilia
uhuru wa mahakama hadi kufikia hatua ya kutoa maelekezo ndani ya mahakama hiyo
kazi ambayo inapaswa kufanywa na afisa wa mahakama na sio jeshi la polisi.
Alisema kuwa kitendo kinachofanywa na jeshi la polisi
kuwanyanyasa wanahabari hakikubaliki katika sheria za nchi na kama utpc
kitazungumza na uongozi wa jeshi la juu la polisi kuhusu hali hiyo kwani
asilimia kubwa ya waliohudhuria kesi hiyo ni askari hivyo kuwaweka katika
wakati mgumu wanahabari kufanya kazi yao kwa waledi.
No comments:
Post a Comment