HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 27, 2016

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA SEKRETARIETI NA WAFANYAKAZI WA CHAMA DODOMA MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt John Pombe Magufuli amekutana na Sekretarieti pamoja na kufanya mazungumzo na watumishi wa Chama cha Mapinduzi ofisi ya Makao Makuu Dodoma na watumishi kutoka Ofisi ndogo ya Lumumba jijini Dar es salaam katika ukumbi wa NEC uliopo Makao Makuu ya CCM, Dodoma.

Kikao hiko baina ya Mwenyekiti mpya wa CCM na Sekretarieti yake mpya aliyoiteua na kuthibitishwa  na Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 23/7/2016 ni Kikao cha kwanza cha utambulisho rasmi na kuweka mpango kazi.

Aidha, Mwenyekiti huyo wa CCM amekutana na watumishi wa CCM wa Ofisi ya Makao Makuu Dodoma na ofisi ndogo ya Lumumba, pamoja na kujitambulisha Dkt Magufuli ameahidi kushughulikia changamoto zote za utumishi ndani ya Chama, ameomba ushirikiano na kusisitiza kujituma na kufanya kazi kwa bidii.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa mara baada ya kuwasili makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
c4.Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akijiandaa kuongea na sekretarieti ya CCM kwa mara ya kwanza katika  makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wafanyakazi wa  makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo
c11: Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Waziri Mkuu Ndg. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Secretarieti ya CCM  makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo.
c14:Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiaga baada ya kupata picha ya pamoja na Sekretarieti ya CCm na wafanyakazi wa makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akisikiliza maoni na changamoto toka kwa wafanyakazi wa  makao makuu ya chama hicho mjini Dodoma leo. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages