Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Ofisi ya TANAPA jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ofisi za TANAPA jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali
Gaudence Milanzi (katikati), akikata
utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
Baadhi ya wadau wa sekta ya Utalii wakiwa katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali
Gaudence Milanzi (katikati), akikata
utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (katikati), akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Tanapa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi akiangalia ofisi mpya ya TANAPA iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi.
Kuangalia ofisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi (kushoto), akifafanua jambo wakati Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kulia) alipokuwa akikagua Ofisi ya Tanapa zilizopo jijijini Dar es Salaam.
Chumba cha mikutano.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Allan Kijazi (kulia), akifafanua jambo wakati Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi (kushoto).
Jengo la Ofisi za TANAPA zilizopo Dar es Salaam.
NA IRENE MARK
MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Allan Kijazi amesema soko kubwa la utalii lipo jijini Dar es Salaam hivyo uongozi wa shirika hilo umeamua kuwasogelea wateja wake kwa kufungua ofisi jijini hapa.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ofisi hizo zilizopo ndani ya jengo la Bodi ya Utalii, alisema hivi sasa wapo kwenye mpango wa kuboresha huduma zao na kufanya utalii wa kisasa huku akiwahakikishia wanaotaka kutembelea hifadhi za wanyama kupata huduma zote katika ofisi hizo mpya badala ya kwenda Arusha kama ilivyokuwa.
“Tumeona kwamba soko kubwa la utalii lipo Dar es Salaam kwa sababu mwaka jana hifadhi tatu za Mikumi, Ruaha na Sadan zilizopo jirani na jiji hili zilitembelewa na watalii wa ndani 54,538 sawa na asilimia 12.6 ya watalii wote wa ndani waliotembelea hifadhi zetu,” alisema Kijazi.
Alisema ofisi hizo zitawapunguzia gaharama ya muda na safari ya kwenda Arusha kwa ajili ya kufanya maandalizi ya safari zao huku akisisitiza kwamba huduma za shirika hilo zimeboreshwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Jenerali Gaudence Milanzi aliyefungua rasmi ofisi hizo aliupongeza uongozi wa TANAPA kwa kuzisimamia vema hifadhi hizo huku akisisitiza kwamba zaidi ya nusu ya watalii wanaoingia nchini, wanatembelea hifadhi za taifa.
“TANAPA mmepewa mamlaka ya kusimamia asilimia 6.1 ya ardhi yote iliyotengwa kwa ajili ya uhifadhi nawashauri sasa muendelee kutumia mbinu za kisasa kupambana na watalii huku mkitafuta njia za kuongeza hamasa za watalii kuja nchini kwa kujitangaza zaidi,” alisisitiza Meja Jenerali Milanzi.
Shirika hilo linalosimamia hifadhi 16 za taifa zilizopo hapa nchini hazijawahi kuwa na ofisi nje ya Jiji la Arusha hivyo ufunguzi wa ofisi hizo ni moja ya njia za kuwasongelea wateja wake uongozi wa Tanapa ukiahidi kufungua ofisi zaidi kwenye majiji.


No comments:
Post a Comment