HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2016

BENKI YA CRDB YADHAMINI BONANZA LA MPIRA WA KIKAPU

 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa CRDB, Tully Esther Mwambapa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bonza la Mpira wa Kikapu kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya CRDB. (Picha na Francis Dande) 
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, akifunga goli kuashiria uzinduzi wa bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Bonanza hilo lilidhaminiwa na benki hiyo.
 Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa CRDB, Tully Esther Mwambapa, akikagua timu katika bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.
 Mchezaji wa Kikapu wa timu ya Libeneke, Edion Brighton (kushoto), akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa timu ya Old Guards, John Tungaraza, katika bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki hiyo.
 Mchezaji wa timu ya mpira wa Kikapu ya Old Guards, Godwin Semunyu, akizongwa na mchezaji wa timu ya Libeneke, Joseph Iyaka katika bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam na kudhaminiwa na Benki ya CRDB.
Na Mwandishi Wetu

WAZAZI wameshauliwa kuwapa nafasi ya kushiriki michezo watoto wao ili kuwajengea utumilifu wa akili kwenye masomo yao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa wateja wa CRDB, Tully Esther Mwambapa kwenye bonanza la mpira wa kikapu lililofanyika jana kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam.

Tully, alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa michezo katika kuboresha afya Benki ya CRDB imetenga kiasi cha asilimia moja ya faida yake kurudisha kwa jamii kupitia huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo.

"Ni vizuri tukawahusisha watoto katika michezo, itawajenga kiakili na kuwa katika nafasi ya kufanya vizuri, si vyema kuwafungia ndani na kutowapa nafasi ya kushiriki michezo na wenzao," alisema Tully.

Bonanza hilo lilishirikisha wachezaji mbalimbali wa mpira wa kikapu wakiwemo watoto ambapo timu za Libeneke, Chang'ombe, Old Guards pamoja na Pazi.

Katika hatua nyingine, Tully alitoa mchango wa Sh. Milioni mbili kwa ajili ya kusaidia kukarabati viwanja vya mchezo huo vya Gymkhana.

No comments:

Post a Comment

Pages