UTANGULIZI
Kitengo
cha dharura cha kuitikia matukio ya
usalama kwenye mitandao nchini (Tanzania Computer Emergency Response Team-
TZ-CERT) kimepewa jukumu la kitaifa la kuratibu matukio ya usalama
katika mitandao kwa kushirikiana na vyombo vingine vya kikanda na kimataifa
katika kusimamia matukio ya usalama mitandaoni.
TZ-CERT ilianzishwa kwa sheria ya Mawasiliano ya
Kielektroniki na Posta ya 2010, kifungu namba 124. Kifungu namba 5(1) cha
kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta zilizotolewa Desemba 2011,
kilielekeza uanzishwaji wa TZ-CERT ndani ya mfumo wa Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA). Huduma za TZ-CERT zilizinduliwa rasmi tarehe 17 mwezi May mwaka 2015.
Majukumu makuu ya TZ-CERT
kisheria ni kuwa kiungo cha kitaifa nchini na kwa nchi za nje kwa masuala yote
yanaohusiana na usalama mtandaoni. Katika kutimiza wajibu wake TZ-CERT:
1.
Inatoa ushauri wa kitaalamu wa kukabiliana na matukio
ya kiusalama yanayotokea na kuzuia madhara zaidi,
2.
Inafanya uchambuzi wa taarifa za matukio ya usalama wa
mtandao kutoka vyanzo mbalimbali, kimataifa na kitaifa,
3.
Kutoa mwongozo wa kitaalamu “Security Advisory” kwa umma na wadau katika maeneo ambayo
yameonekana kuwa na madhaifu,
4.
Uhamasishaji, kuelimisha na kujenga uwezo (Awareness & Capacity Building) wa
masuala ya usalama wa mitandao kwa serikali na wadau kutoka
sekta mbalimbali.
5.
Tathimini ya udhaifu wa
mifumo ya kompyuta (Vulnerability
assessment) katika mitandao ya wadau wa TZ-CERT.
Ikumbukwe kwa sasa Tanzania
kuna watumiaji wa mtandao wanaokadiriwa kufikia milioni Kumi na Saba (17 milioni) kutokea milioni Tano (5 milioni) katika mwaka 2011.
Kutokana na uzoefu
uliopatikana kwa muda wa mwaka mmoja toka ianze rasmi kutoa huduma, TCRA imebaini
pamoja na mambo mengine ukosefu wa taarifa muhimu za usalama wa mitandaoni
kumechangia kuwepo kwa matukio ambayo yangeweza kuepukika.
2.
Kwa nini kampeni ya kuongeza ufahamu?
Kampeni hii ya kuongeza ufahamu imekuja wakati
muafaka baada ya timu ya TZ-CERT kubaini changamoto nyingi na aina mbalimbali
za matatizo ya kwenye mtandao ambayo wanakutana nayo watanzania wengi kutokana
na ufahamu mdogo wa jinsi ya kujilinda mitandaoni, kulinda taarifa zao
mtandaoni pamoja na matumizi sahihi ya mtandao kwa ujumla wake.
3.
Kampeni itawalenga watu gani?
Kampeni hii inawalenga watumiaji wa huduma za
Intaneti wa rika zote kuanzia watoto mpaka watu wazima.
4. Kampeni
itahusisha nini?
Kampeni hii inazinduliwa rasmi leo tarehe 17 mwezi
8 mwaka 2016 na itaendelea kwa miezi mitatu. Hata hivyo kampeni za kuelekea
uzinduzi wa leo zilianza tarehe 01 Agosti, 2016. Kwa kuwa kampeni hii ni ya matumizi ya mitandao
itaendeshwa zaidi kwenye mitandao ambapo watumiaji wa mitandao mbali mbali
Tanzania watatumia muda wao kujifunza njia bora na salama za matumizi ya
mtandao.
Katika kipindi hiki cha kampeni wananchi
watajifunza mada mbali mbali ikiwa ni pamoja na matunzo sahihi ya kompyuta na
programu zake, taratibu za kutumia mitandao kwa usalama, matumizi sahihi ya
namba au neno la siri, sheria ya makosa ya mitandao, uwekaji wa taarifa kwenye
mitandao ya kijamii na matumizi sahihi ya mitandao kwa watoto.
Kampeni hii itatolewa katika akaunti za TZ-CERT za
mtandao wa facebook (https://www.facebook.com/Tz-Cert), twitter (https://twitter.com/tz_cert) na instagram (https://www.instagram.com/), pamoja na vyombo vya redio na TV kufikisha jumbe
mbalimbali za kuelimisha watumiaji wa mitandao na umma matumizi sahihi ya mitandao.
5.
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA
UTUMIAPO HUDUMA ZA INTANETI/MITANDAO
i.
Kuwa makini na taarifa za binafsi unazoziweka kwenye mitandao wa jamii,
ii.
Ukisaidiwa
kuanzisha akaunti za mtandao wa kijamii, hakikisha unabadilisha neno la siri lilotumika
mara moja na neno hilo la siri usimshirikishe mtu yeyote,
iii.
Usijibu jumbe unazopokea
kwenye akaunti yako ya barua pepe unaokutaka kuhakiki taarifa zako,
iv.
Usijibu ujumbe wowote wa barua pepe unaokueleza kuwa umeshinda bahati nasibu,
v.
Usifungue kiambatisho au
kubofya kiungo (link) unayotumiwa na mtu usie mjua kabla ya kuhakikisha uhalali
wa barua pepe husika.
Ili kujiepusha na kukiuka
sheria mbalimbali za mawasiliano ya mtandao umma wote unashauriwa kuzingatia
yafuatayo:
i.
Usitunge na kusambaza ujumbe wa maudhi, uzushi au
uchochezi,
ii.
Usiendelee kusambaza ujumbe wa chuki, maudhi au uchochezi
unaopokea kutoka kwa mtu mwingine. Badala yake ufute mara uupokeapo au toa
taarifa,
iii.
Usitembelee
tovuti na blogu za ponografia/ngono,
iv.
Usitengeneze
akaunti za mitandao ama kwa lengo la kufanya utapeli, ulaghai au kwa kutumia taarifa
zisizo zako,
v.
Tunza vifaa unavyohifadhia kumbukumbu zako.
6
Uzinduzi wa tovuti mpya ya
TZ-CERT
Pamoja na uzinduzi wa kampeni hii, pia tovuti mpya
ya TZ-CERT itazinduliwa rasmi leo. Tovuti hii yenye lugha ya kingereza na
Kiswahili itaanza kutumika rasmi kutoa taarifa muhimu za kuwasaidia wananchi
kujilinda na matukio ya kwenye mitandao. Tovuti hii pia hutumika kutuma na kutoa
taarifa ya matukio mbali mbali kwa TZ-CERT kwa msaada wa kitaalamu. Anwani ya tovuti hizi ni www.tzcert.go.tz
Imetolewa na:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
Mawasiliano Towers
20 Bara Bara ya Sam Nujoma
S.L.P. 474
14414 DAR ES SALAAM
17 Agosti 2016
No comments:
Post a Comment