Na Mbaruku Yusuph, Muheza
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tanga kimewaonya wananchi wilayani Muheza kutoingia kwenye mtego wa kuhatarisha amani iliyopo nchini kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoani humo Rajab Abdurahman, alipokuwa akizungumza na wananchi katika Kata ya Nkumba Wilayani Muheza ambapo ni mwendelezo wa ziara yake ya kampeni kuelekea uchaguzi huo.
Komred Rajab alisema Tanzania imeendelea kuwa nchi yenye utulivu kutokana na amani iliyojengwa na waasisi wa Taifa, hivyo chama hicho hakitakubali kuona watu wachache wakijaribu kuivuruga kwa maslahi binafsi.
“Hembu ndugu zangu, tukumbuke jinsi wananchi kutoka nchi jirani kama Burundi na Rwanda walivyoteseka kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tuchukue tahadhari ili tusije tukajikuta sisi tukipoteza amani yetu na kuwa wakimbizi,” alisema Kambaredi Rajab.
Aliongeza kuwa siku ya Oktoba 29 ni muhimu kwa wananchi kote nchini, akiwahimiza kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuichagua CCM katika nafasi za udiwani, ubunge na urais, kwa kuwa ndicho chama pekee kinachoweza kulinda na kudumisha amani iliyopo.
Kwa upande wake, Balozi Adadi Rajabu, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Muheza (2015–2020), aliwaonya wananchi wasipotoshwe na watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuhamasisha maandamano siku ya uchaguzi, akisema vyombo vya ulinzi na usalama viko imara na vitahakikisha hakuna vurugu zozote.
“Ni jambo la kushangaza kuona watu wanaoshawishi maandamano wakiwa nje ya nchi. Hawa watu wanapaswa kupuuzwa kabisa, vyombo vya ulinzi na usalama viko tayari, na hakuna maandamano yatakayofanyika,” alisema Balozi Adadi.
Aidha, aliwataka wananchi wa Muheza wasiwe na hofu, bali wajitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi, akisisitiza kuwa serikali itahakikisha usalama wao unaimarishwa ipasavyo.
“Nilipokuwa katika taasisi za kiusalama, tulishuhudia baadhi ya maandamano yakigeuka na kuleta madhara. Baadhi ya washiriki walikamatwa na kufungwa, huku waliowachochea wakikimbia. Hivyo, ni muhimu tujifunze kutokana na historia hiyo tusije tukaingia kwenye mtego huo tena,” aliongeza Balozi Adadi.
Akizungumza katika mkutano huo mgombea Ubunge wa jimbo hilo la Muheza Hamisi Mwinjuma (mwana FA)ikiwa ni mwendelezo wa kampeni kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 alisema ccm ndio Chama pekee chenye lengo kuu la kushughulikia matatizo ya wananchi.
Mwinjuma alisema historia ipo wazi tangu muungano wa TANU na ASP hatimae CCM kazi kubwa ni kuwatumikia wananchi kuwaletea maendeleo na kutatua kero zinazowakabili wananchi.
"Niwaambie tu ndugu zangu baada ya Oct 29 vyama vyote vitapotea na Ccm ndio chama kitakachobakia kupana na kero za wananchi"Alisema Mwana FA.
Hata hivyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa kata hiyo ya Nkumba wazijotokeze kwa wingi Oct 29,2025 kwa ajili ya kuwapigia kura wagombea toka CCM kwa nafasi ya udiwani,ubunge na Rais.




No comments:
Post a Comment