Timu ya Golf ya Jeshi ya Lugalo imetakiwa kuhakikisha inawapa raha wanachama wake akiwemo Mlezi wa Klabu hiyo ambaye ni Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali davis Mwamunyange kwa kurejesha Ubingwa wa mashindano ya Moshi Open mashindano yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo wakati akiongea na Wachezaji hao katika mazoezi yao ya Mwisho katika Klabu ya Lugalo Jijini Dar es Salaam kabla ya Kuondoka kuelekea Moshi.
"Hakuna sababu kwa Timu ya Jeshi iliyofanya mazoezi kwa muda Mrefu ikashindwa kirahisi katika Mashindano kama haya ambayo tuliwahi kuchukua ubingwa kiukweli wapeni raha wanachama wenu" Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.
Aliongeza kuwa Wanachama wa Lugalo akiwemo Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara hawahitaji kitu kingine zaidi ya Furaha ya Ushindi ambayo watakuwa wanaifuatilia hivyo ni Jukumu la wachezaji hao kuhakikisha wanakamilisha Furaha hiyo.
Pia aliwataka wanachama wa Golf kuhakikisha wanamtuma kazi ili kuhakikisha mafaninio makubwa yanapatikana ikiwemo kuboresha Uwanja wa Golf wa Lugalo ambao ni Uwanja uliojengwa na wazalendo kuwa Bora na kuhamasisha Mashindano mengi ya Kimataifa kuandaliwa katika Uwanja huo.
Mwenyekiti huyo ambaye ameteuliwa hivi karibuni aliahidi kuboresha Klabu hiyo na kuifanya kuwa ya kisasa zaidi na Kuwa kiwanja bora Afrika Mashariki na kuwataka watu wote kujitokeza kushiriki katika mchezo huo kwani ni mchezo unaokubalika kwa rika zote.
Kwa upande wake Kapteni wa Timu hiyo Kapten Kassim Usitambe alisema Mara baada ya Mashindano hayo watakayoshiriki wakiwa ni wachezaji Tisa kutoka klabu ya Lugalo wataelekea Mkoani Arusha kwa mashindano ya Tanzania Open.
Kwa upande wake mmoja wa wapiga Gofu hao Amina Hamisi aliahidi kurejea na ushindi katioka mashindano hayo ili kutoa zawadio kwa mwenyekiti mpya ikiwa ni siku chache tu baada ya kuteuliwa kushika madaraka hayo.
Timu hiyo ya Golf iliyoondoka leo (Agosti Nne) itashiriki Mashindano hayo ya Moshi Open ambayo Klabu hiyo Mwaka 2014 walichukua kikombe yatashirikisha Wachezaji wote wakiwemo wa Nje sambamba na ya Tanzania open ambayo wapiga Gofu kutoka Nje ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment