Raia wa Kenya, John Osodo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi (kulia) alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika Jijini Mwanza.
Dkt. Frank Mgeta wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure (kulia), akipata maelezo mbalimbali yanayohusu mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, jijini Mwanza.
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leonard Chamurho (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leornard Chamurho (kushoto), akifurahia maelezo yanayotolewa na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
Mhandisi Diana Munubi (wa kwanza kulia) akitoa maelezo yaliyomfurahisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dtk. Leonard Chamuriho (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo na Afisa Usafirishaji Mkuu wa Uchukuzi, Alphonce Mwingira katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) kutoka taasisi za TAA, TCAA, TMA na DMI wanaoshiriki kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, linalofanyika Mwanza, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamurho, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Prof. Faustine Kamuzora, na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.
No comments:
Post a Comment