Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, kushoto
akifurahia jambo katika Sikukuu ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa
nchini humo kwa kukutanisha Watanzania wanaoishi Saudi Arabia, wazawa na
viongozi mbalimbali kama sehemu ya kuitangaza vyema Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania. Kwa hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.
Na Mwandishi Maalum, Riyadh Saud Arabia
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza wa nane kutoka
kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali katika maadhimisho ya
Sikukuu ya Muungano nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kusherehekea
pamoja katika siku hiyo muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.
Balozi Mgaza akiwa na mgeni rasmi Prince Muhammad bin abdullahman wakikata keki ya sherehe.
Balozi Mgaza akihutubia katika hafla hiyo
Alisema
kutokana na sera hizo pamoja na kusimamia vyema rasilimali za utalii
kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga mbalimbali za wanyama ni sehemu
thabiti ya utalii kwa wageni, wakiwamo wananchi wa Saudi Arabia.
“Nchi
yetu ina mbuga za wanyama 16 ambazo zimekuwa zikitunzwa na kuhifadhiwa
vema kama sehemu ya kuhakikisha kwamba rasimali hiyo inakuza uchumi wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Nchi yetu ina
wakaribisha wote kutembelea kujionea mambo mbalimbali yanayovutia katika
utalii pamoja na kuwekeza katika sekta muhimu zikiwamo za viwanda
ambazo ndio agenda kuu kwa sasa nchini mwetu,” Alisema Balozi Mgaza.
Sikukuu
ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeadhimishwa wiki
iliyopita Aprili 26 ambayo hutumiwa kama kioo cha kuangalia matunda
yanayojitokeza kutokana na Muungano huo kati ya Tanzania Bara na
Visiwani.
No comments:
Post a Comment