HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 09, 2017

MVUA ZASABABISHA FAMILIA ZAIDI YA ELFU TATU KUKOSA MAKAZI PEMBA

Naibu katibu CUF Nassor Ahmed Mazurui akizungumza akichukua maelezo kutoka kwa Bi Maariam Suleiman ambaye nyumba yake ilifukiwa na kifusi cha udongo katika Kijiji cha Jondeni Wilaya ya mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.  (Picha na Talib Ussi).
 Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazurui akizungumza na waathirika wa mafuriko katika Kijiji cha Muambe Kisiwani Pemba.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazurui akizungumza na waathirika wa mafuriko katika Kijiji cha Muambe Kisiwani Pemba.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazurui akitembelea eneo lililopatwa na mafuriko katika Kijiji cha Muambe Kisiwani Pemba. 

Na Talib Ussi, Zanzibar

Jumla ya Nyumba 666 zimeathiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha Kisiwani Pemba huku nyumba 200 zikisombwa kabisa na kuziacha familia zaidi ya 3000 kukosa makazi.

Hayo yalidhihirikia jana baada ya Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF Nasor Ahmed Mazurui kufanya ziara maalum ya kuwafariji waathirika hao.

Wakizungumza na kiongozi huyo katika Kijiji Cha Muambe Mkoa wa Kusini kisiwani walisema sababu kubwa ni mvua lakini wakadaii na uzembe wa Serikali kwa kuchimba Fusi kwa ajili ya kutengenezea barabara kasha na kuliyaacha mashimo ambayo yamejaa maji.

“Mh. Japo mvua ni sababu lakini Serikali imechangia kwani tuliwaeleza kuwa wasituchimbie fusi karibu na majumba lakini hawakukubali,leo hii maji yamejaa hayana njia yamekuja majumbani mwetuu” alieleza Seif Khamis Mohammed ambaye ni mkaazi ya kijiji hicho.

Mohammed alifahamisha kuwa katika eneo hilo Nyumba 62 zimeanguka kutokana mvua hizo na wakaazi wake kupewa makaazi katika majengo ya Afisi tofauti zikiwemo za CUF.
Aidha alieleza khofu yao kubwa ni kukumbwa na maradhi mripuko hasa kipindupindu kutokana kuzagaa kwa uchafu uliozagaa maeneo hayo.

Shauri Makame Khamis alieleza kuwa katika mashimo hayo walijaribu kupanda migomba lakini haikuwa na msaada kwa tukio hilo.

“Sisi tumejaribu kutaka kulizuia lakini , juhudi zetu ni za kimasikini kwa hiyo hatukufanikiwa” alieleza Khamis.
Kufuatia maelezo hayo Naibu huyo aliwataka wananchi kuwaangalia wezao waliopatwa majanga hayo ili wajione kuwa msiba huo ni wao wote.

Pia aliwaomba kila mwenye uwezo aweze kutoa msaada wa hali na Mali hasa katika kipindi hichi kwani hawana hata chakula.

“Tunayaomba mashirika ya kutoa misaada kuwaangalia kwa haraka wananchi hawa kwani hali zao ni mbaya sana na wako katika hali ya kimasikini sana” alieleza Mazurui.
Sambamba na hilo Mazurui aliwaomba wananchi hao kuwa na ustahamilivu na wasijewakajenga katika maeneo ambayo makazi yao yalibomoka kwa ambacho mvua inaendelea kunyesha.

Aidha aliwaomba wannachi kuwa kazi ya kwanza aliifanya ni kufanya tathimini na muda mmfupi tena kwa haraka wataweza kutoa msaada wao ili kupunguza machungu ya athari hizo.

Kwa upande wake Bi Mariam Khamis wa kijiji cha Jondeni ambaye Nyumba yake iliporomokewa na Mlima alifahamisha kuwa anamshukuru mola wake kwani wakiwa wamelala ndio nyumba yao iliangukiwa na mlima kutokana na mvua kubwa na kupelekea watu wote kufukuwa.
“Tulikuwaa watu 5 sote tulifukuwa lakini majirani walisikia mshindo ndio wakafanya jithada za kutuokoa na Alhamdulillah wazima ispokuwa mwezetu mmoja hajatoka hospitali lakini naye anendelea vizuri”

Bi Ziada omari ambaye ni alisikia kishindo cha kuanguka mlima huo na kutoka nje ndio akaona hali ilivyokuwa na kupiga kalele na kuwamsha majirani na kueleza kuwa wakati huo mvua ilikuwa inanyeesha sana.

Rashid Ghalid ambaye ni mkazi wa Micheweni alieleza kuwa katika Wilaya yao hiyo Nyumba 59 zimebomoka moja kwa moja kutokana na mvua hizo.

Alimueleza mazurua kuwa wanasikitika licha ya hali mbaya ambayo wananchi imewapata hakuna hata kiongozi mmoja aliyefika angalau kuwafariji.

“Lakini juhudi zetu wananchi zimepelekea wenzetu kuwasaidia kwa kuwapatia huduma tofauti ambazo zimo kwenye uwezo wetu” alieleza Rashid.

Ama kwa upande wilaya za wete na chake chake Nyumba 79 zimeangukaa na kuwaacha wenyewe wakihangaika kutafuta wasamaria weme waweze kuwahifadhi.

Wataalamu Kisiwani humo wameleza kuwa hali ya mvua hiyo haijawahi kunyesha karibuni miaka 30 iliyopita.

No comments:

Post a Comment

Pages