HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 28, 2017

Taasisi ya Women On Wheel - Africa yatoa mafunzo ya udereva kwa wanawake

AF1
Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akizungumza na wanawake akina mama kwa wasichana wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya udereva wa kibiashara ambao utawawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.
Bw. Martin Gabone amesema Semina hii ina lengo la kuwaandaa wanawake watanzania na Afrika kwa ujumla kupata ujuzi katika taaluma ya udereva wa kibiashara ambapo wanawake hawa watapata mafunzo maalum katika programu ya Women On Wheel - Africa ili kujiwezesha na kujitegemea kiuchumi kupitia taaluma hii ya udereva wa kibiashara na wenye tija kwa maisha yao na taifa kwa ujumla wake.
Women On Wheel - Africa inawakaribisha wanawake akina mama kwa wasichana kujisajiri ili kujiunga na mpango huu muhimu ambapo mafunzo yanatarajiwa kuanza mwezi wa tisa mwaka huu 2017 jijini Dar es salaam katika ofisi za taasisi ya
Kwa mawasiliano zaidi unaweza kutumia namba hizi
OFISI ZA TAASISI HIYO ZIPO KINONDONI ADA ESTATE KARIBU NA BAKWATA HIGH SCHOOL
AF3
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ofisi za Women On Wheel - Africa Kinondoni.
AF4
Baadhi ya washiriki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ofisi za Women On Wheel - Africa Kinondoni.
AF5
Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanawake akina mama kwa wasichana wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.
AF7
Mjasiriamali Bi Tedy Daniel mmoja wa washiriki wa semina hiyo akifafanua jambo kwa wanasemina wenzake wakati wa mafunzo hayo.
AF8
Bw. Martin Gabone Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Women On Wheel - Africa akiwaelekeza jambo baadhi ya washiriki wakati wa semina ya iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwapa mafunzo ya ujasiriamali na kuwawezesha kiuchumi kupitia sekta ya usafirishaji.

No comments:

Post a Comment

Pages