HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 24, 2017

MICHUANO YA SOKA LA UFUKWENI KUTIMUA VUMBI NOVEMBA 19

NA MAKUBURI ALLY

KAMATI ya Soka la Ufukweni limeandaa ligi inayotarajia kuanza Novemba 19, uwanja wa Karume Ilala jijini Dar es Salaam itakayoshirikisha wachezaji kutoka vyuo mbalimbali vya elimu hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa Ligi hiyo, Deo Lucas alisema mwaka huu wamejipanga kushirikisha vyuo 50 hapa nchini.

Lucas alisema ameshawasilisha mialiko kwa vyuo mbalimbali ambavyo vinatakiwa kujitokeza kuchukua fomu za ushiriki wa ligi hiyo.

Aidha Lucas alisema baada ya ligi hiyo kumalizika, wanajipanga kuandaa ligi itakayofanyika Desemba mwaka huu ambayo itashirikisha timu za mitaani ambazo zitapambana vilivyo kwa ajili ya kusaka timu bora ya Tanzania itakayoshiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa.

Lucas alisema wameandaa mashindano hayo kwa sababu Tanzania ipo katika nafasi nzuri katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) ambako iko katika nafasi ya 12 duniani huku namba moja ikishikiliwa na Brazil.

No comments:

Post a Comment

Pages