HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

October 24, 2017

TIKETI SIMBA, YANGA MWISHO IJUMAA

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza taratibu za uuzaji wa tiketi kwa ajili ya mchezo kati ya Simba na Yanga limeanza leo hadi Ijumaa unaotarajia kuchezwa Oktoba 28 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema siku ya mchezo, tiketi hazitouzwa hivyo alitoa wito kwa mashabiki na wapenzi wa soka Tanzania kununua mapema tiketi hizo.

“Tunawaomba mashabiki na wapenzi wa soka wa Simba na Yanga kununua tiketi mapema kabla ya mchezo ili kufanikisha mchezo huo kuchezwa kwa utulivu wa aina yake,” alisema Lucas.

Aidha Lucas alisema viingilio vya mchezo huo kwa VIP ni shilingi 20,000 na viti vya kawaida shilingi 10000.

No comments:

Post a Comment

Pages