HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 06, 2017

IHD kujadili maendeleo ya elimu ya awali

 Mmoja wa washiriki akichangia mada.
 Mratibu wa Taasisi ya Maendeleo ya Binadabu (IHD) Leonard Chumo (kushoto ) akizungumza kuhusu kongamano la kimataifa kujadili maendeleo ya elimu ya awali. kulia ni Profesa Kofi Marfo. 
Wadau wa Masuala ya watoto.

NA HAPPINESS MNALE

CHUO Kikuu cha Aga Khan kupitia Taasisi yake ya Maendeleo ya Binadamu (IHD) imeandaa kongamano la pili la kimataifa kuhusu maendeleo ya elimu ya awali.
Kongamano hilo linaanza kesho ambapo linafanyika kwa mara kwanza jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waaandishi wa habari Mratibu wa IHD, Leonard Chumo, alisema kwamba kongamano hilo litajadili fursa za maendelo ya elimu ya awali katika maeneo yenye kipato cha chini.

Chumo alisema kwamba kongamano hilo litaanza kesho na kumalizika Novemba 9,mwaka huu.

Alisema kwamba kongamano hilo la kimataifa litawashirikisha watafiti wa elimu, watekelezeji wa programu, wataalamu wa elimu na watunga sera.

“Kongamano limejikita katika maudhui ya maendeleo ya elimu ya awali katika nyakati zisizo na uhakika; kuanzia uelewa na ushahidi katika kujitolea na utekelezaji,”alisema.
Alisema kwamba washiriki wa kongamano hilo watanufaika na utafiti na programu ya IHD ambayo inaimarisha ubora wa maisha ya watoto. 

Aidha alisema kwamba litasaidia kujenga ushiriki wa wazazi na wataalamu wa elimu ambao ni msingi wa kumpa kila mtoto kiu ya kujifunza.

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibanyila, alisema kwamba ni vyema wazazi wakajenga tabia ya kuzungumza na watoto wao ambao hawajafikia umri wa kuzungumza ili kuwajenga kiakili na kuwaweka karibu.

Alisema kwamba wazazi wengi wanaweka mbele kipaumbele cha kazi hali inayowanyima fursa watoto.

“Jamii pia ijifunze kuwalinda watoto iache unyanyasaji kwa watoto, ihakikishe mtoto anapata lishe bora ili awe na afya,”alisema Dk. Neema

No comments:

Post a Comment

Pages