Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt.
Mussa Mgwatu kushoto akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa bodi ya Ushauri ya wakala
huo Mhandisi Brig. Gen. (Mstaafu) Mabula Berthiraya Mashauri kulia mwenye
miwani wakati alipofanya ziara katika karakana ya Mt Depot jijini Dar es Salaam
kujionea utendaji kazi wa Karakana hiyo mapema leo.
Meneja wa Karakana ya Mt Depot Mhandisi Julius Humbe (wa pili
kulia) akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Mhandisi Brig. Gen. (Mstaafu) Mabula Berthiraya Mashauri (wa
tatu kulia) wakati alipokua katika ziara ya kujionea utendaji kazi wa karakana hiyo
jijini Dar es Salaam mapema leo. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na
Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu.
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Mhandisi Sylvester Simfukwe aliyenyoosha mkono akimuonyesha
kifaa cha kunyanyulia gari wakati wa matengenezo (car lifter) Mwenyekiti wa
bodi ya Ushauri ya wakala huo Mhandisi Brig. Gen. (Mstaafu) Mabula Berthiraya
Mashauri (wa pili kulia) wakati wakati alipokua katika ziara ya kujionea
utendaji kazi wa karakana hiyo jijini Dar es Salaam mapema leo. Kulia ni Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu.
Mafundi wa karakana ya Mt Depot wakiipima vilainishi gari ya
serikali iliyopelekwa katika karakana hiyo na kuifunga mara baada ya kumaliza
kuifanyia matengenezo ya kawaida. PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA).
No comments:
Post a Comment