HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2017

KUWAIT YAZINDUA MPANGO KAMILI WA KUWASAIDIA WALEMAVU TANZANIA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya watu wenye ulemavu katika Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana , kulia ni Balozi wa Kuweit nchini Tanzania, Jasem Al-Najem.
Balozi wa Kuweit nchini Tanzania, Jasem Al-Najem akizungumza jambo katika hafla fupi ya kumkabidhi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kushoto) vifaa mbalimbali kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni msaada kutoka serikali ya Kuweit, hafla iliyofanyika jana katika Chuo Cha Ufundi Cha Yombo kinachotoa mafunzo kwa Walemavu, Dar es Salaam jana, wakwanza kushoto ni Katibu Muhutasi wa Balozi na wakwanza kulia ni Mkalimani wa Balozi, Abdallah Yahaya.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi cherehani, Lenah Sauli (kushoto).


Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa kwanza kushoto), wakati mmoja wa mwanafunzi wa Chuo hicho, Lenah Sauli alipokua akishona nguo.

Na Maria Inviolata

SERIKALI ya Kuwait kwa kupitia Ubalozi wake nchini umezindua mpango kamili wa kuwasaidia watu wenye ulemavu nchini Tanzania katika Chuo Cha Ufundi Yombo jijini Dar es salaam.

Uzinduzi huo uliofanyika juzi ulihudhuriwa na Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem Al-Najem, waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera,Bunge,Kazi,vijana,Ajira na walemavu Mhe. Jenista Mhagama,Kaimu wa Chuo Bi Maryam, walimu na wanafunzi,wafanyakazii wa chuo hicho, Mpango huo utahisisha Bara na Visiwani.

Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Al-Najem katika hotuba yake wakati wa uzinduzi huo amesema kuwa mpango huo utagharimu kiasi cha dola laki 5 sawa na shilingi bilioni 1.1 utaendeshwa nchi nzima kwa awamu kwa kushirikiana na maafisa wa Serikali ya Tanzania na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.

Chuo cha wenye ulemavu Yombo kimemepata msaada wa zaidi ya Milioni 26,098,125. Pamoja na vyerehani vitatu, dazeni mbili za mafuta ya maalum ya wenye ulemavu wa ngozi. Balozi Al-Najem alimkabidhi Waziri Mhagama vifaa vya wenye ulemavu ,kama vile vifaa kwa wasioona, viti vya matairi, fimbo maalum za kuwaongoza wenye ulemavu wa macho,,magongo,miwani,vifaa vya kuwasaidia wenye udhaifu wa kusikia ilihali Balozi huyo akiahidi kuchangia vifaa vya upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa katika Taasisi ya Mifupa MOI.

Sanjari na uzinduzi huo uliokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 3 mwezi wa 12, katika salamu zake kwa siku hiyo Balozi huyo ambaye ndiye mlezi wa Chuo cha Wenye Ulemavu Yombo anatoa rai kwa kila mwanadamu kujitolea ili kuhakikisha Wenye Ulemavu wanatimiza malengo yao.

Kwa upande wake waziri mwenye dhamana Mhe.Jenister Mhagama amesema kuwa tanzania itaendelea kutekeleza maazimio ya kimataifa kuhusu walemavu huku akiyataka mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na sekta binafsi kuiga mfano wa Serikali ya Kuwait, watu wake na Ubalozi wake hapa nchini katika kuwasaidia walemavu.

Aidha Waziri Mhagama ameishukuru Serikali ya Kuwait kwa misaada hii na kuuomba Ubalozi kusaidia katika kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili chuo cha Ufundi Yombo kama vile uchimbaji wa kisima na makazi kwa wanafunzi walemavu.

Chuo hicho kiko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu, kilianzishwa mwaka 1973, malengo yakiwa ni kutoa mafunzo ya stadi za Kazi kwa watu wenye ulemavu ili waweze kujitegemea na kufanya shughuli za kujiingizia kipato ili kuepukakuwa tegemezi.

Chuo hicho kina uwezo wa kuingiza wanafunzi 150 kwa wakati mmoja ila kwa sasa kina jumla ya wanafunzi 63 wenye ulemavu wa aina mbalimbali mathalani viziwi,albino,wenye ulemavu wa viungo, akilina uoni.

Aidha Cho hicho kinatoa Elimu ya mafunzo ya ufundi stadi katika fani mbalimbali, kwa sasa ni fani za umeme wa majumbani, uungaji vyuma, kilimo na ufugaji,ushonaji,nguona ujenzi, huduma za marekebisho na utengamano (Reahabiliaition).

No comments:

Post a Comment

Pages