HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 06, 2017

MAFUNZO YA UFUNDI STADI YATAKUZA UCHUMI WA VIWANDA-VETA

 Msanii wa Vichekesho Emanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Kanda ya Dar es Salaam.
 Msanii wa vichekesho Emanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ akipata maelezo mafupi juu ya namna mafunzo ya ufundi stadi yanavyotolewa na Mamlaka ya Mafunzo na UFundi Stadi (VETA) Kanda ya Dar es Salaam.
 NA JANETH JOVIN

MAMLAKA ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema kuwa uchumi wa viwanda hauwezi kukua bila ya kuwa na wataalamu wa kutosha wa ufundi stadi hivyo imeitaka jamii kuondokana na dhana potofu ya kuamini kuwa mafunzo wanayoyatoa ni ya kundi maalumu.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam jana na Meneja Mahusiano wa VETA, Sitta Petter wakati wa ziara ya Mchekeshaji maarufu Nchini, Emanuel Mathias ‘Mc Pilipili’ alipoitembelea mamlaka hiyo.

Petter alisema ni vema jamii ikatambua kuwa ufundi stadi ni jambo muhimu katika nchi hasa nyakati hizi ambazo Serikali ya awamu ya tano imejipambanua katika uchumi wa viwanda.

Alisema suala la ufundi stadi linamchango mkubwa katika kuinua uchumi wa viwanda na kuwafanya watu hasa vijana kujiajiri na kuondokana na dhana ya kuajiriwa kama ilivyo kwenye fani nyingine wanazosomea.

“Katika dunia ya sasa mtu ambaye ana uhakika na ajira ni yule aliyesomea ufundi stadi, hii ni kwa sababu anaujuzi mkubwa wa kufanya kazi ya mikono hivyo ni rahisi kuweza kujiajiri mwenyewe kwa hapa kwetu suala hili la ufundi ni la muhimu sana kwani tunaelekea katika uchumi wa viwanda,” alisema.

Naye Mc Pilipili alisema ametembelea vyuo mbalimbali vya VETA na amejionea jinsi ambavyo vinafanya kazi kubwa ya kutoa mafunzo hayo kwa vijana hivyo wanapaswa kupongezwa.

No comments:

Post a Comment

Pages