Kocha
wa timu ya Taifa ya soka la ufukweni, John Mwansasu ameita wachezaji 16
watakaoingia kambini kesho Jumamosi Desemba 16, 2017 kujiandaa na
michuano ya Copa Dar es Salaam itakayofanyika kwa siku mbili kwenye
Ufukwe wa Coco.
Kikosi
hicho cha wachezaji 16 kitaingia kambini kwa muda wa wiki nzima
kujiandaa na mashindano hayo ya kimataifa yatakayojumuisha timu nne
ambazo ni Malawi, Uganda, Zanzibar na wenyeji Tanzania Bara.
Wachezaji
walioitwa ni pamoja na Rajabu Ghana (Huru), Khalifa Mgaya (Chuo cha
CBE), Juma Kaseja (Kagera Sugar), Juma Sultan (Chuo Kikuu Ardhi), Ally
Rabby (Huru), Mwalimu Akida (Huru), Samwel Salonge (Huru), Athuman Idd
'Chuji' (Coastal Union), Kenan Mwandisi (Huru), John Pauseke (Huru),
Joseph Jafet (Huru), Jaruph Rajab Juma (Chuo cha DIT), Mbwana Mshindo
(Chuo cha DSJ), Rolland Msonjo (Singida United), Jerry Francis Robert
(Huru) na Haruna Moshi (Friends Rangers)
Benchi
la ufundi linaongozwa na Mwansasu mwenyewe akisaidiwa na kocha wa
makipa Peter Manyika, Meneja Deo Lucas na daktari wa timu Richard Yomba.
Kocha
John Mwansasu amesema mashindano hayo ya Copa Dar Es Salaam
yatakayofanyika Desemba 25 na 26, 2017 yatasaidia kuwaongezea uzoefu
zaidi kwa mchezo huo wa soka la Ufukweni.
No comments:
Post a Comment