HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 19, 2017

TUZO ZA ATE, SSRA YAIBUKA KIDEDEA MWAJIRI BORA SEKTA YA UMMA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akikabidhi kwa SSRA Tuzo ya Mwajiri Bora kwa Mwaka 2017. Anayepokea ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Lightness Mauki.
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu Bw. Eric Shitindi akikabidhi kikombe kwa SSRA baada ya kuibuka mwajiri bora wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za Mwajiri bora wa Mwaka 2017 zilizotolewa hivi karibuni na Chama cha Waajiri Nchini (ATE) jijini Dar es Salaam. Anayepokea ni Mkurugenzi wa SSRA Bi. Lightness Mauki.

Watumishi wa SSRA wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuibuka mshindi wa jumla kwa Taasisi za Umma katika hafla ya utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2017 zilizotolewa na Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA Bi. Sarah Kibonde Msika (kulia), akiwa kwenye Meza ya SSRA, wakati wa hafla ya utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2017 zilizotolewa na Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wafanyakazi wa SSRA wakiwa kwenye meza ya SSRA wakati hafla ya utoaji Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2017 zilizotolewa na Chama cha Waajiri Nchini (ATE) Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Pages