NA SHEHE SEMTAWA
KLINIKI
ya Matumaini Heberisti imewataka wanandoa wanaosumbuliwa na tatizo la
uzazi waache kusononeka, baadala yake wafike katika kituo hicho ili
aweze kupatiwa tiba ya kumaliza tatizo hilo.
Mmiliki
wa kituo hicho, Tausi Kagunduka, aliyasema hayo baada ya kubaini kuwa
wapo wanandoa wengi ambao wameigia katika migogoro ya kifamilia kutokana
na kukosa watoto kwa muda mrefu tangu walipofunga ndoa.
Akizungumza
na Habari Mseto jijini Dar es Salaam leo,Tausi alisema Kiliniki hiyo
imejipanga kusaidia baadhi ya wanandoa wanaokabiliwa na tatizo hilo,
ambalo kwa sasa anaamini linaweza kutibika.
Alisema,
ameweka wazi kuwa tatizo hilo linaweza kutoweka kwa wanandoa endapo
watatumia dawa ya Engelo ambayo ilivumbuliwa na kliniki hiyo na
kuthibitishwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto
miaka sita iliyopita.
"Dawa
hiyo pamoja na milinolino zilithibitishwa kwa kumbukumbu Namba
341/VOLXIII/11/40 na Namba TBB/SLM.II/KNG.II pamoja na LAB No.341/2011,
hata hivyo kwa kila hatua tunayofanya tunawasiliana na Ofisi ya Mkemia
Mkuu wa serikali.
"Mimi
nashauri mwenye tatizo hilo aje au ni vema wahusika wakafika kwenye
kliniki yetu pamoja ili wote waweze kupata tiba, tunafanya hivyo kwa
sababu tatizo hilo linaweza kujitokeza kwa yeyote kati yao bila
kujijua,"alisema Tausi.
Tausi,
alisema licha ya kutibu magonjwa mbalimbali ikiwemo upungufu wa kinga
mwilini, lakini amebaini kuwa wagonjwa wengi wanaojitokeza katika
kliniki hiyo ni wanawake wanaokabiliwa na tatizo la uzazi.
"Unajua
mafanikio katika tiba hiyo yatasaidia kuimarisha ndoa za watu kwani
kuna baadhi ya ndoa zilivunjika kutokana na kukosa watoto, kwa hiyo
nawaomba wafike Buguruni Marapa karibu na kanisa la mabati na kisha
wanipigie simu namba 0717303050 na 0784624554,"alifafanua Tausi.
Akizungumzia kuhusu dawa ya mlinolino, Tausi, alidai dawa hiyo inatibu maradhi mbalimbali ikiwemo upungufu wa kinga mwilini.
Alidai
kuwa tangu wagonjwa wake walipoanza kuitumia dawa hiyo, kwenda kupimwa
hospitalini baadhi yao yawalidai kwamba waligundulika kuwa wamepona.
"Tangu
nimeanza dawa ya mlinolino kutibu watu wenye upungufu wa kinga mwilini
sijapata msukosuko wowote kutoka serikalini kwani baada ya kuwapatia
matibabu hayo nawashauri waende Hospitali kwa ajili ya kufanyiwa
uchunguzi kuona kama wamepona au la,"alisema Tausi.
Aidha,
Tausi alisema Kliniki hiyo pia imekuwa ikitoa msaada wa matibabu bure
kwa watoto ambao wazazi wao wamefariki kutokana na maradhi ya ukimwi.
Aliongeza
kuwa gharama za matibabu hayo kwa watu wazima ni sh.200,000 huku
akibainisha kuwa waliweka bei hiyo ili kila mwenye tatizo hilo aweze
kupata matibabu.
No comments:
Post a Comment