HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 25, 2017

UBALOZI WA KUWAIT NCHINI TANZANIA WATOA MSAADA KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM MKOANI TABORA

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Dk. Amon Mkoga, Bwana Amon Mkoga (kulia), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum. Katikati ni Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Stella Ikupa, akifuatiwa na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al Najem. Ubalozi wa Kuwait umetoa vyerehani, fimbo za kutembelea walemavu na baiskeli za walemavu vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 18 kwa watu wenye mahitaji maalum kutoka mkoa wa Tabora. (Na Mpiga Picha Wetu).
Naibu Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mhe. Stella Ikupa (wa pili kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jasem Al Najem (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Taasisi ya Dk. Amon Mkoga (kulia), pamoja na watoto wenye mahitaji maalum.
Baadhi ya vifaa vilivyotolewa na ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya watuy wenye mahitaji maalum mkoani Tabora.

No comments:

Post a Comment

Pages