Dar es Salaam, Tanzania
Kaimu Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndugu Daniel Zenda akikabidhi kadi 1500 za wanachama wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kwa Katibu wa Hamasa Seneti ya mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Juakali Kuwanya katika hafla iliyofanyika leo Makao Makuu ya UVCCM, Upanga jijini Dar es Salaam.
Zenda amesema, kadi hizo amezikabidhi ili zigawiwe kwa wananchama wapya ambao wamekuwa wakijiunga kwa wingi katika Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake, kutokana na mwamko mkubwa wa wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuunga mkono CCM kutokana na kuvutiwa na Utendaji kazi wa Rais John Magufuli na Serikali yake ya awamu ya tano
Imetolewa na
Uvccm Seneti Mkoa Dsm.
No comments:
Post a Comment