Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na uongozi wa Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu,
wakati alipofanya ziara ya kukagua miradi ya miundombinu ya barabara mkoani
humo. Wa Kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Seif Shekalaghe.
Muonekano wa sehemu
ya barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3 ambayo ujenzi wake
umekamilika kwa asilimia 98, mkoani Simiyu. Ujenzi huo umefadhiliwa na Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 na umegharimu kiasi cha
shilingi bilioni 61.46.
Gari maalum
likimwaga lami ya mwisho katika barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3, wilayani
Maswa, Mkoani Simiyu. Ujenzi wa barabara hiyo umegharimu Serikali kiasi cha shilingi
bilioni 61.46.
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akisisitiza
jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt. Seif Shekalaghe kuhusu umuhimu wa
kutunza barabara ya Mwigumbi-Maswa KM 50.3 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango
cha lami, wilayani humo, mkoani Simiyu,
Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipokea
taarifa ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Mwigumbi-Maswa yenye urefu wa KM 50.3
kutoka kwa Meneja Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Simiyu, Mhandisi
Albert Kent (wa pili kulia), mara baada ya kukagua hatua iliyofikiwa ya ujenzi
wa barabara hiyo, wilayani Maswa, mkoani Simiyu.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment