WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na
kumpa pole Mwenyekiti wa Chama Cha Walimu (CWT) mkoa wa Singida Mwalimu Aron
Jumbe aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Akiwa hospitalini hapo leo (Jumamosi, Februari 10, 2018), Waziri Mkuu amefarijika baada ya kumkuta Mwenyekiti huyo na wagonjwa wengine waliolazwa kwenye taasisi hiyo wakihudumiwa vizuri.
Pia Waziri Mkuu amewajulia hali mabinti
pacha walioungana Consolata na Maria Mwakikuti ambao nao wamelazwa katika Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI).
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa hao na kuwaeleza kwamba Serikali inadhamira
ya dhati kuhakikisha inaboresha huduma za afya na kwamba madaktari wataendelea
kuwahudumia vizuri ili kuhakikishia afya zao zinaimarika na kurejea katika shughuli zao za kila siku
Kwa upande wake,
Mwalimu Jumbe alimshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kwenda kumjulia
hali. Aliwashukuru madaktari na wauguzi wa taasisi ya JKCI kwa huduma nzuri
wanazompatia tangu alipofika hospitalini hapo.
Kwa upande wao Maria
na Consolata walishukuru kwa msaada wa huduma za matibabu wanazozipata na kwa
sasa wanaendelea vizuri. Pia walimshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kuwajulia hali na kumtakia kheri katika shughuli
zake
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, FEBRUARI 10,
2018.
No comments:
Post a Comment