HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 04, 2018

TUSIKATE MITI OVYO-MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Zanzibar kuacha kukata miti ovyo kwa kufanya hivyo wataharibu historia ya Zanzibar kwa kuondoa Viumbe adimu na uoto wa asili.

Aliyaeleza hayo huko Sheheia ya Fuoni kibondeni Wilaya ya Magharib Unguja ikiwa ni muendelezo wake wa ziara ya siku tatu Visiwani Zanzibar.

Alieleza kuwa kuna kila sababu jamii kujikita katika utunzaji wazingira ikiwemo upandaji wa miti sambamba na kutunza uoto asili wa bahari.


“Mola wetu alituumbia dunia na miti ili tuishi katika Maisha ya salama leo mkiamua kukata miti ndio mnahatarisha Maisha ya watu” alieleza Bi Samia.


Sambamba na hayo aliwataka wananchi kufahamau kuwa uharibufu wa mazingira ni kuharibu maisha ya watu waliopo sasa na vizazi vitakavokuja.

Mapema Mwaka Masoud, ambaye ni katibu wa kikundi cha utunzaji Mazingira katika shehia hiyo alifahamisha kuwa kutokana binaadamu kukata miti kwa wingi Viumbe vya Baharini vilikuwa vinatoweka pampja na uonto wa asili.

“Lakini baada ya kupanda miti , tumefanikiwa kuzuia hali na sasa mazingira yetu kiasi Fulani yanapendezaa” alieleza Mwaka.

Alimueleza Makamo huyo kuwa kwa sasa wanakabiliwa na Changamoto bado wananchi wanendelea kuharibu mazingiraa kutokana na kukata miti ovyo kwa kuni na ujenzi na kumuomba wapatiwe boti ya doria.

No comments:

Post a Comment

Pages