Meneja
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kulia), akimkabidhi
Ganiya Shabani zawadi ya simu janja aina ya Tecno R6 aliyoshinda katika
promosheni inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus huku akitazamwa na baadhi
ya washindi wengine wa promosheni hiyo. Tigo imetoa jumla ya simu 676
bure pamoja na bonasi za intaneti hadi GB 1 kwa wateja wake walionunua
bando za intaneti kupitia menu yake iliyoboreshwa ya *147*00#.
Dar es Salaam, Tanzania
Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini
ya Tigo Tanzania inazidi kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za intaneti
nchini baada ya kuwazawadia wateja wake 676 simu janja aina ya Tecno R6 katika
promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus.
Katika promosheni hii murwa ambapo Tigo inatoa
jumla ya simu janja 12 kila siku, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za
intaneti za kuanzia TSH 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# pia
wanapata bonasi ya hadi GB 1 bure kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter.
‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo
unaoendana na maslahi na mahitaji ya wateja ili kuwezesha kila mtu kufurahia
maisha bora ya kidigitali kupitia mtandao wetu mpana wa Tigo,’ Meneja
Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael alisema katika hafla fupi ya kuwakabidhi
washindi simu zao jijini Dar es Salaam leo.
Akizungumza katika hafla
kama hiyo iliyofanyika mjini Morogoro leo, Mtalaam wa Usambaji Bidhaa wa Tigo, Baraka
Hamza alisema kuwa kupitia promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo
inafanikisha azma yake ya kuwaunganisha wananchi wote na mtandao wake wenye
kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G.
‘Tunataka kila mtu awe sehemu ya mabadiliko makubwa
yanayotokana na kuunganishwa na mtandao wa intaneti na pia kufurahia huduma
bora zenye uwezo wa kubadili maisha zinazotopatikana katika mtandao wetu wenye
kasi ya juu na mpana zaidi nchini wa Tigo 4G unaopatikana katika miji 24
nchini,’ alisema.
Takwimu za hivi karibuni zilizotolewa na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa asilimia 45% tu ya Watanzania ndiyo
waliofikiwa na huduma za kimtandao, huku asilimia 84% ya wale waliofikiwa
wakitumia simu zao za mkononi kama njia kuu ya kupata huduma hizo za mtandao. Ubunifu
huu wa Tigo utahakikisha kuwa idadi ya watumiaji wa huduma za mtandao
inaongezeka nchini.
‘Tunawaasa wateja wetu kuchangamkia fursa hii kubwa
ya kuwa sehemu ya mageuzi ya ulimwengu wa kisasa wa kidigitali kwa kununua
bando intaneti kupitia *147*00# ili wajipatie bonasi za intaneti pamoja na
nafasi ya kujishinidia simu janja aina ya Tecno R6 kutoka Tigo.’ Woinde alibainisha.
No comments:
Post a Comment