NA
SULEIMAN MSUYA
MTANDAO
wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), umetoa msaada wa unga wa muhogo tani 1.7
zenye thamani ya Sh. Mil 3.5 kwa Kituo cha Kulea watoto yatima Hananasifu
(Hocet).
Msaada
huo huo wa unga umekabidhiwa kwa Hocet na Mwenyekiti wa Bodi ya Mkiita, Dk.
Kissui Kissui jana jijini Dar es Salaam.
Alisema
wameamua kusaidia kituo hicho kama sehemu ya mchango wao kwa jamii na kwamba
kiasi hicho ni sehemu ya mavuno ya kwanza ya uwekezaji wao katika kilimo hicho.
Dk.
Kissui alisema Mkikita wamelima muhogo katika
maeneo ya Bagamoyo, Mkuranga na Kisarawe.“Tumelima muhogo katika
mashamba yetu tumevuna na baada ya kusaga tumepata tani 15 hivyo tumekubaliana
kutoa tani 1.7 Hocet ili vijana waweze kupata chakula kwa siku chache kwani ni
wadau wetu,” alisema.
Mwenyekiti
huyo alisema pamoja na msaada huo wa chakula kwa Hocet wanaamini kuwa kupitia
wao watakuwa wamefikisha ujumbe kwa jamii kuhusu kufanya kilimo chenye tija
zaidi.
Mkurugenzi
wa Mkikita, Adam Ngamange alisema wametoa msaada huo kwa kituo cha watoto
yatima wakiamini kuwa ni sehemu sahihi hata kwa maagizo ya Mungu.
“Mungu
ameagiza yatima wasaidiwe na sisi katika mavuno yetu ya kwanza tangu kuanza
kuwekeza wenyewe tumeona tuanze na vijana hawa ambao wanahitaji msaada na
biashara itafuata,” alisema.
Ngamange
aliwataka wakulima nchini kutumia Mkikita katika kutafua masoko ya bidhaa zao
kwani uhakiki wa kupata soko ni mkubwa kutokana na mtandao waliona duniani.
Alisema
Mkikita inajihusha na kilimo cha muhogo, papai, pilipili kichaa na mazao
mengine ambayo yamekuwa yakihitajika katika nchi mbalimbali kama China, Uturuki
na Ujerumani.
Mwanzilishi
wa Hocet, Hezekia Mwalugaja, alisema msaada huo ni muhimu katika kituo chao na
kwamba utataweza kusaidia changamoto ya chakula.
Mwalujaga
alisema Mkikita imechagua sehemu sahihi katika kutoa msaada huo wa unga kwani
ni dhahiri kituo kinahitaji na kuwataka wadau wengine kuinga mfano huo.
“Kimsingi
hamjakosea kuja Hocet kwani tunawahitaji sana watu kama nyie lakini pia katika
kituo tunafundisha masomo ya kilimo hivyo tunaenda pamoja kimtazamo na kupitia
nafasi hii vijana watakuwa wamemahasika,” alisema.
Kwa
upande wake Hamida Shaaban, mmoja wa watoto katika kituo hicho alisema msaada
huo umesababisha watambue kuwa wapo watu wanaowajali kutokana na hali zao.
No comments:
Post a Comment