Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 (Ngorongoro
Heroes) itacheza na timu ya Taifa ya Mali U20 Jumapili Mei 13,2018 Uwanja wa
Taifa Dar es Salaam.
Katika mchezo huo utakaochezwa saa 10 jioni kiingilio cha
kuingia Uwanjani kutazama mechi hiyo VIP zote shilingi 3,000 Mzunguko shilingi
1,000.
Ngorongoro Heroes wapo kambini wakiendelea kujiandaa na
mchezo huo,leo wapo kwenye ratiba ya kufanya mazoezi ya gym asubuhi na jioni
kabla ya kuwa na mazoezi ya uwanjani kesho na Ijumaa ambapo kesho Alhamisi watakuwa
na kipindi kimoja cha Uwanjani saa 10 kwenye Uwanja wa Uhuru wakati Ijumaa
watafanya vipindi viwili asubuhi na jioni saa 10.
Kikosi hicho hakina majeruhi vijana wana morali kubwa ya
kufanya vizuri katika mchezo huo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu fainali
za vijana Africa.
LIGI
YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA KUTIMUA VUMBI MEI 6,2018
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa(RCL) inatarajia kuanza kutimua
vumbi kuanzia Jumapili Mei 6 na kumalizika Mei 22,2018 kwenye vituo vinne.
Ligi hiyo ya RCL itashirikisha timu 28 zilizogawanywa
kwenye makundi manne kwenye vituo vya Geita,Singida,Rukwa na Kilimanjaro na
kila kundi kwenye kituo likiwa na timu 7.
Kila kundi litapandisha timu 2 wakati zitakazobaki zitarudi
ligi ya mkoa.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF
No comments:
Post a Comment