Jamii imeshauriwa kuwa na utaratibu wa kupanda miti
kwenye maeneo yao ili kuhifadhi na kutunza
mazingira kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyoathiri
makaazi ya watu kwa kasi.
Ushauri huo ulitolewa na Waziri wa Elimu na mafuzo ya Amali Riziki
Pembe Juma huko Kitope wilaya kasakazini B Unguja wakati akizindua mpango
maalumu wa Chuo cha teknologia ya biashara (Microtech) wa kupanda miti zaidi ya
alfu 20 katika shule zote za Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alieleza hivi sasa maeneo mengi watu wameyahama kutokana makaazi
yao kuvamiwa na maji ya bahari na kudai kuwa yote hayo yamesababishwa na
ukataji miti ovyo ikiwemo mikoko ambayo ipo kwa ajili ya kuzuia mawimbi ya
bahari.
“Tupandeni miti kwa ajili ya kulinda mazingira yetu ambayo
yatatuwezesha kupata hewa safi na kuepuka baadhi ya maradhi” alieleza Bi Riziki
Pembe.
Alieleza kuwa kupanda miti ni sawa na kutowa sadaka kwa kile alichokifahamisha kuwa wazee
walipanda miti miaka mingi iliyopita na hadi leo watu wanaitumia.
“Leo tunakula matunda aina tofauti hii sadaka yenye kuendelea
ambayo ilipandwa na mababu na bibi zetu karne kwa karine basin a sisi
tuapandeni tukijua kuwa kesho mbele ya mola wetu tunalofungu na hapa duniani
tunalinda afya zetu” alieleza Waziri huyo.kuiga upandaji wa miti hiyo.
Aidha wakati akizindua kampeni hiyo aliwataka wanafunzi wa Shule ya Kitope
kuitunza miti hiyo wasome wakiwa katika mazingira salama.
Mkurugenzi wa chuo hicho ambacho kipo Magomeni Zanzibar Said
Saleh Mohamed, alisema
wameamuwa kufanya kazi hiyo kwa sababu bila ya kuwepo mazingira bola hakuna
Afya na kama hakuna afya hapana elimu bora.
“Tunawaambia Jamii yetu ya Tanzania kwa ujumla kuwa sisi hatupo
kwa biashara pekee bali ni pomoja na kulinda maisha yaliotuzunguka”alieleza
Mkurugenzi huyo.
Pia aliitumia fursa hiyo kufiomba vyuo vyengine
kuunga mkono kampeni hiyo ili zanzibar na Tanzania iweze kuwa na mazingira
salama.




No comments:
Post a Comment